title : WAHAMIAJI HARAMU 72 NA WAKALA WAO WAKAMATWA PWANI
kiungo : WAHAMIAJI HARAMU 72 NA WAKALA WAO WAKAMATWA PWANI
WAHAMIAJI HARAMU 72 NA WAKALA WAO WAKAMATWA PWANI
Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
JESHI la Polisi Mkoani Pwani ,linamshikilia mfanyabiashara anaedaiwa kuwasafirisha wahamiaji haramu 72 raia kutoka nchini Ethiopia,Rajabu Hitaji (30)mkazi wa Vigwaza ,Bagamoyo . Aidha jeshi hilo linawashikilia pia wahamiaji haramu hao kwa kosa la kuingia nchini bila kibali .
Akitolea ufafanuzi juu ya tukio hilo ,kamanda wa Polisi mkoani Pwani(ACP) Jonathan Shanna ,alisema uchunguzi unaendelea na watafikishwa ofisi za uhamiaji kwa hatua nyingine stahiki.
Alieleza ,mtuhumiwa Hitaji ambae ni mfanyabiashara alikamatwa jana, saa 3.30 asubuhi huko maeneo ya pori la ranchi ya Taifa Narco ,Vigwaza wilaya ya kipolisi Chalinze .
“Kufuatia msako mkali ulioendeshwa na makachero wetu baada ya kupata taarifa juu ya uwepo wa raia walioingia nchini pasipo kufuata taratibu za uhamiaji na raia hao baada ya kugundua kuna gari la polisi linawafuatilia “
“Waliingia kwenye hifadhi hiyo kwa lengo la kujificha lakini askari wetu waliweza kubaini mahali walipo kufuatia msako mkali uliokuwa ukiendeshwa katika ranchi hiyo ” alisema kamanda Shanna .
Hivyo makala WAHAMIAJI HARAMU 72 NA WAKALA WAO WAKAMATWA PWANI
yaani makala yote WAHAMIAJI HARAMU 72 NA WAKALA WAO WAKAMATWA PWANI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAHAMIAJI HARAMU 72 NA WAKALA WAO WAKAMATWA PWANI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/08/wahamiaji-haramu-72-na-wakala-wao.html
0 Response to "WAHAMIAJI HARAMU 72 NA WAKALA WAO WAKAMATWA PWANI"
Post a Comment