title : Upandaji miti maskulini kusaidia changamoto za kimazingira
kiungo : Upandaji miti maskulini kusaidia changamoto za kimazingira
Upandaji miti maskulini kusaidia changamoto za kimazingira
Na Habiba Zarali, Pemba
OFISA Mdhamini Wizara ya Ardhi,Maji ,Nishati na Mazingira Pemba, Juma Bakar Alawi, amesema utamaduni ulioanzishwa na Wanafunzi wa upandaji miti maskulini, kutasaidia kuzipatia ufumbuzi changamoto mbalimbali za kimazingira zilizopo katika maeneo yao wanayojifunzia pamoja na maeneo wanayoishi.
Kauli hiyo aliitowa katika hafla ya kukabidhi zawadi kwa Skuli za Sekondari ya Kangani na Skuli ya msingi Makombeni Wilaya ya Mkoani Pemba, ambazo ni miongoni mwa Skuli zilizofanya vizuri katika mradi wa mazingira maskulini “ECO SCHOOLS”inayofadhiliwa na Zayadesa na kutekelezwa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar.
Alisema mradi huo ni miongoni mwa hatuwa zinazochukuliwa katika kutekeleza kwa vitendo malengo endelevu ya sasa ya dunia, pamoja na utekelezaji wa lengo ambalo linahusika na utowaji wa elimu stahiki ya maendeleo endelevu ya rasilimali hiyo.
Alifahamisha udumishaji wa mazingira ikiwemo kupanda miti ni hazina kubwa iliyotoka kwa wazee ambao waliweza kuilinda na kuiendeleza hadi kufikia leo hii, sasa basi ni jukumu la vizazi vya sasa kuona umuhimu
huo ambao utasaidia matumizi endelevu ya rasilimali hiyo, ili vizazi vijavyo navyo viweze kufaidika.
“Wanafunzi mradi huu ni fursa kwenu wala musione kama ni utumwa kwani upandaji wa miti ni usafi wa mazingira ambao hata dini ya kiislamu imehimiza na kusema muislamu ni usafi”alisema.
Alifahamisha ili nusra iweze kupatikana kwa kuepusha mmong’onyoko ,maporomoko na maji ya bahari kupanda juu ni jukumu la jamii kuwa mstari wa mbele kupanda miti kwa wingi, sambamba na kupeana elimu ambayo itasaidia kuwashajihisha wale ambao bado uwelewa wao ni mdogo.
“Nyinyi wanafunzi ambao tayari mumeshapata mafunzo ya utunzaji wa mazingira kupitia Skuli zenu, sasa mutowe elimu majumbani ili nako jamii iweze kuelewa umuhimu wa utunzaji wa mazingira “alisema.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa ECO SCHOOLS Zanzibar , Abdul-Aziz Mohammed Iddi , akitowa taarifa kuhusu mradi huo, alisema utawapatia nchi wanachama fursa za kuitambuwa ,kuziendeleza na kuzitekeleza njia ,mbinu na dhana za kukabiliana na changamoto endelevu za kimazingira kama vile mabadiliko ya tabia nchi ,matumizi ya rasilimali ,majanga ya kimaumbile ,udhibiti wa taka na uharibifu wa matumbawe.
Alisema Skuli kupitia mradi huo zina fursa kufanya kazi kwa pamoja katika kukabiliana na matatizo yanayozikabili nchi zinazoendelea za Visiwa vidogo vidogo kwa kuungwa mkono na jumuiya ya kimataifa kwa kupata zawadi mbalimbali.
“Kwa kuwa mradi huu ni endelevu mwelekeo wake basi ni ushiriki wa wote ambapo uhamisho au kustafu kwa mwalimu au kumaliza Skuli kwa baadhi ya wanafunzi hakuwezi kuathiri uwepo wake”, alisema.
Mapema wakisoma risala ya eco program, Skuli ya Kangani walisema baada ya kuingia katika mradi huo wamepata mwamko mpya juu ya uhifadhi wa mazingira ,kuimarisha usafi wa Skuli pamoja na jamii zao ,kujifunza
mambo mbalimbali ya asili kama vile kupiga kumba na madawa ya asili waliokuwa wakitumia wazee wao.
Walisema hadi sasa wanahifadhi mazingira ya bahari kwa lengo la kuzuwia mmong’onyoko wa ardhi na kuzuwia maji chumvi kuingia katika mashamba na makaazi ya watu.
Jumla ya Skuli 30 teule za Serikali na za binafsi kutoka Zanzibar zinatekelezwa na mradi huo, ambapo kwa Unguja ni 21 na Pemba ni 9, na Skuli 12 ikiwemo ya Sekondari Kangani na msingi Makombeni zimeweza kufikia viwango vya kujipatia tunzo mbalimbali zikiwemo Ngao za Shaba na za Dhahabu.
Hivyo makala Upandaji miti maskulini kusaidia changamoto za kimazingira
yaani makala yote Upandaji miti maskulini kusaidia changamoto za kimazingira Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Upandaji miti maskulini kusaidia changamoto za kimazingira mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/08/upandaji-miti-maskulini-kusaidia.html
0 Response to "Upandaji miti maskulini kusaidia changamoto za kimazingira"
Post a Comment