UJENZI WA BOMBA LA MAFUTA GHAFI: MRADI WENYE FURSA KEDEKEDE WATANZANIA WANAPASWA KUZICHANGAMKIA

UJENZI WA BOMBA LA MAFUTA GHAFI: MRADI WENYE FURSA KEDEKEDE WATANZANIA WANAPASWA KUZICHANGAMKIA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa UJENZI WA BOMBA LA MAFUTA GHAFI: MRADI WENYE FURSA KEDEKEDE WATANZANIA WANAPASWA KUZICHANGAMKIA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : UJENZI WA BOMBA LA MAFUTA GHAFI: MRADI WENYE FURSA KEDEKEDE WATANZANIA WANAPASWA KUZICHANGAMKIA
kiungo : UJENZI WA BOMBA LA MAFUTA GHAFI: MRADI WENYE FURSA KEDEKEDE WATANZANIA WANAPASWA KUZICHANGAMKIA

soma pia


UJENZI WA BOMBA LA MAFUTA GHAFI: MRADI WENYE FURSA KEDEKEDE WATANZANIA WANAPASWA KUZICHANGAMKIA

Hivi Karibuni, Rais wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli na Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda kwa pamoja waliweka jiwe la msingi la Ujenzi wa Bomba la Mafuta Ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Tanga Tanzania. Katika Makala hii pamoja na mambo mengine Mwandishi Said Ameir wa Idara ya Habari- MAELEZO anaeleza kwani nini mradi huu ni kipimo cha utayari na ujasiri wa watanzania katika kuchangamkia fursa.

Mradi huu unaojulikana kama Mradi wa Bomba la Kusafirisha Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) unatekelezwa kwa ubia kati ya washirika wa sekta binafsi na sekta za umma za nchi za Tanzania na Uganda.

Washirika hao ni Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Kampuni ya Taifa ya Petroli ya Uganda (UNOC), Kampuni ya Mafuta ya Total ya Ufaransa, Kampuni ya TULLOW yenye makao makuu yake London nchini Uingereza na Kampuni ya China National Offshore Oil Company (CNOOC).

Bomba ambalo litagharimu dola za kimarekani 3.5 bilioni, sehemu yake kubwa yaani kilomita 1,115 kati ya kilomita 1,445 litajengwa katika ardhi ya Tanzania na kupita mikoa 8, wilaya 24 na vijiji 184.

Kutokana na hali hiyo, inaelezwa kuwa, mradi huu wakati wa ujenzi na utakapokamilika, utatoa na fursa nyingi za kiuchumi ambazo zitasaidia sana kuchangamsha shughuli za kiuchumi hivyo kuchangia ukuaji uchumi na kuinua kiwango cha maisha ya watanzania kwa namna mbalimbali.

Mradi huu ni mfano wa ushirikiano kati ya nchi za Tanzania na Uganda na kwa upande mwingine ni mfano mzuri wa ushirikiano kati ya sekta binafsi na sekta za umma katika nchi hizi. 

Katika hatua mbalimbali za utekelezaji wake, mradi huu utahitaji ushiriki wa sekta binafsi katika nchi zote mbili na wakati mwingine hata taasisi nyingine za umma ambazo zinatoa huduma zitakazohitajika na mradi.

Kwa hiyo, wakati tukisifia kuwa ni mfano wa mradi wa ubia wa sekta ya umma na sekta binafsi katika nchi zetu, watanzania hawana budi kuelewa kuwa wana wajibu mkubwa wa kuzitumia vyema fursa za mradi huu.

Kwa Tanzania, mradi huu unaweza kuonesha picha halisi ya ushirikiano wa sekta hizo kwa kuzingatia namna makampuni na taasisi za humu nchini zitakavyoweza kushiriki na kufanikisha mradi huu.

Kwa maana nyingie ni mradi ambao unaweza kutumika kupima utayari, umakini, uwezo na ujasiri wa watanzania katika kuchangamkia fursa za kiuchumi.



Hivyo makala UJENZI WA BOMBA LA MAFUTA GHAFI: MRADI WENYE FURSA KEDEKEDE WATANZANIA WANAPASWA KUZICHANGAMKIA

yaani makala yote UJENZI WA BOMBA LA MAFUTA GHAFI: MRADI WENYE FURSA KEDEKEDE WATANZANIA WANAPASWA KUZICHANGAMKIA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala UJENZI WA BOMBA LA MAFUTA GHAFI: MRADI WENYE FURSA KEDEKEDE WATANZANIA WANAPASWA KUZICHANGAMKIA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/08/ujenzi-wa-bomba-la-mafuta-ghafi-mradi.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "UJENZI WA BOMBA LA MAFUTA GHAFI: MRADI WENYE FURSA KEDEKEDE WATANZANIA WANAPASWA KUZICHANGAMKIA"

Post a Comment