title : Tunawashukuru wote kwa maombi yenu- Manusura Lucky Vicent
kiungo : Tunawashukuru wote kwa maombi yenu- Manusura Lucky Vicent
Tunawashukuru wote kwa maombi yenu- Manusura Lucky Vicent
Watoto watatu wa shule ya msingi ya Lucky Vicent ambao walinusurika katika ajali ya shule hiyo ya jijini Arusha waliopelekwa nchini Marekani kutibiwa wamerejea nchini jana na kusema wanamshukuru Mungu na pia wanawashukuru watu wote kwa kuwaombea.
Mapokezi ya kuwapokea watoto hao ambao ni Doreen Mshana, Wilson Tarimo na Sadya Awadhi yalifanyika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) na kuhudhuriwa na watu mbalimbali.
Mtoto Wilson “Tunaishukuru serikali ya Tanzania kwa kutusaidia kupata hati za kusafiria sisi na wazazi wetu, lakini pia daktari na muuguzi ambao tulisafiri nao. Sina mengi ya kusema ila nawashukuru kwa sala na dua zenu kwani tuliondoka tukiwa kwenye machela na leo tumerejea tukiwa tunatembea wenyewe,” alisema Wilson.
Mtoto Doreen alisema: “Nawashukuru wote kwa maombi yenu maana hali yangu ilikuwa mbaya kuliko wenzangu, naomba muendelee kuniombea.Nawashukuru madaktari wa Tanzania na Marekani wamenisaidia sana maana sikuwa na fahamu kwenye viungo vya mwili wangu lakini leo hii ni mzima, naomba muendelee kuniombea”.
Kwa upande wa Sadya kwa upande wake alisema hana neno la shukrani zuri zaidi ya asante na kwamba Mungu ni mweza wa yote kwani amefanya mema katika maisha yake na aliwashukuru madaktari waliowasaidia hadi kurejea wakiwa salama.
Ajali hiyo ilitokea, Mei 6 mwaka huu katika ajali hiyo wanafunzi 32 wa darasa la 7, walimu 2 na dereva wa gari la shule hiyo walipoteza maisha.
Hivyo makala Tunawashukuru wote kwa maombi yenu- Manusura Lucky Vicent
yaani makala yote Tunawashukuru wote kwa maombi yenu- Manusura Lucky Vicent Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Tunawashukuru wote kwa maombi yenu- Manusura Lucky Vicent mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/08/tunawashukuru-wote-kwa-maombi-yenu.html
0 Response to "Tunawashukuru wote kwa maombi yenu- Manusura Lucky Vicent"
Post a Comment