title : TTCL YAZINDUA HUDUMA YA 4G LTE MBEYA
kiungo : TTCL YAZINDUA HUDUMA YA 4G LTE MBEYA
TTCL YAZINDUA HUDUMA YA 4G LTE MBEYA
KAMPUNI ya Simu Tanzania (TTCL) imezindua huduma mpya ya mawasiliano ya 4G LTE pamoja na kutambulisha huduma nyingine ya TTCL PESA.
Hata hivyo katika uzinduzi huo imeelezwa kuwa mawasiliano bora yanahitajika ili kuendelea kuimarisha shughuli za kiuchumi mkoani Mbeya ikiwa ni pamoja na kuongeza urahisi wa upatikanaji wa taarifa za masoko na bei nzuri kwa wazalishaji na Wakulima.
Hayo yalielezwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla wakati akizindua huduma mpya ya kampuni ya Simu ya TTCL ya 4G LTE katika hotuba yake iliyosomwa na Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Paul Ntika katika ofisi za Kampuni hiyo zilizopo jijini Mbeya.
Alisema mawasiliano bora yanamchango mkubwa katika ukuaji wa sekta za Elimu, Afya, Miundombinu, Biashara, utalii, huduma za jamii na sekta zingine mtambuka hivyo kitendo cha TTCL kuibuka upya kutasaidia kuchochea maendeleo katika Mkoa wa Mbeya na Taifa kwa ujumla.
Aliongeza kuwa mbali na Mawasiliano kusaidia kukuza uchumi pia Wafanyakazi wa Sekta binafsi na sekta za umma wanahitaji mawasiliano bora ili kuongeza ufanisi wa utendaji kazi na utekelezaji wa majukumu yao katika maeneo yao ya kazi.
Aidha alitoa wito kwa wakazi wa Mkoa wa Mbeya kuchangamkia fursa za kibiashara zinazotolewa na TTCL kama vile kuwa wakala wa kuuza vocha, Laini na kuwa Wakala wa huduma mpya ya kifedha ya TTCL Pesa kwani kufanya hivyo kutasaidia kuongeza ajira na vipato vyao.
Hivyo makala TTCL YAZINDUA HUDUMA YA 4G LTE MBEYA
yaani makala yote TTCL YAZINDUA HUDUMA YA 4G LTE MBEYA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TTCL YAZINDUA HUDUMA YA 4G LTE MBEYA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/08/ttcl-yazindua-huduma-ya-4g-lte-mbeya.html
0 Response to "TTCL YAZINDUA HUDUMA YA 4G LTE MBEYA"
Post a Comment