Tanzania ya Kwanza Kutumia Mfumo wa PlanRep Kusini mwa Afrika

Tanzania ya Kwanza Kutumia Mfumo wa PlanRep Kusini mwa Afrika - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Tanzania ya Kwanza Kutumia Mfumo wa PlanRep Kusini mwa Afrika, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Tanzania ya Kwanza Kutumia Mfumo wa PlanRep Kusini mwa Afrika
kiungo : Tanzania ya Kwanza Kutumia Mfumo wa PlanRep Kusini mwa Afrika

soma pia


Tanzania ya Kwanza Kutumia Mfumo wa PlanRep Kusini mwa Afrika

Tanzania imetajwa kuwa nchi ya kwanza Kusini mwa Afrika kuanza kutumia  mfumo wa kielektroniki wa PlanRep ulioboreshwa ambao husaidia katika mipango, bajeti na kutoa taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo nchini kote.

Akizungumza katika mahojiano maalum mjini Kigoma, Mkuu wa Timu ya Mifumo ya TEHAMA kutoka mradi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)  Desderi Wengaa, amesema kuwa  mfumo huo utasaidia Taifa kufikia maendeleo endelevu kwa wakati kwani utaunganishwa na mifumo mingine iliyopo sasa na utawashirikisha wananchi wote.

“Mfumo huu utawezesha kutolewa kwa taarifa za miradi ya maendeleo zinazohusu sekta zote zilizoainishwa katika mipango na bajeti kwa wakati katika kipindi chote cha mwaka” alisema Wengaa.

Aliendelea kusema kuwa PlanRep iliyoboreshwa inaunganisha sekta zote katika mfumo mmoja ambao ni wa kitaifa tofauti na ilivyokuwa awali ambapo kila sekta ilikuwa na mfumo wake. Awali mfumo uliokuwa ukitumika haukuwa unaendana na mahitaji ya wakati hivyo kushindwa kufanya uchambuzi wa kina katika kusimamia rasilimali zilizokuwepo ikiwemo fedha. 

Aidha,watumiaji wa mfumo huo  wataweza kuutumia mahali popote  kwa kuwa ni wa kitaifa na utaondoa changamoto ya kuwepo kwa matoleo tofauti tofauti. Hali hii itasaidia kuokoa fedha nyingi zilizokuwa zikitumika kwa watoa huduma wa mifumo ya awali katika halmashauri na mikoa yote nchini.
Kiongozi wa Timu ya wataalamu wanaofanya maboresho ya mfumo wa kielektroniki wa PlanRep, Bi. Nseya Kipilyango akizungumza wakati wa mafunzo kwa watumiaji wa mfumo huo yanayoendelea Mjini Kigoma.
Mmoja wa Wawezeshaji wa Mfumo wa mfumo wa kielektroniki wa PlanRep Kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Bi Jacqueline Manyanga akiwasilisha mada kwa watumiaji wa mfumo huo yanayofanyika Mkoani Kigoma yakihusisha Mikoa ya Rukwa, Katavi na Kigoma.
Washiriki wa Mafunzo wakifuatilia mada wakati wa mafunzo hayo yanayoendelea mjini Kigoma.




Hivyo makala Tanzania ya Kwanza Kutumia Mfumo wa PlanRep Kusini mwa Afrika

yaani makala yote Tanzania ya Kwanza Kutumia Mfumo wa PlanRep Kusini mwa Afrika Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Tanzania ya Kwanza Kutumia Mfumo wa PlanRep Kusini mwa Afrika mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/08/tanzania-ya-kwanza-kutumia-mfumo-wa.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Tanzania ya Kwanza Kutumia Mfumo wa PlanRep Kusini mwa Afrika"

Post a Comment