title : NBS YAWATAKA WADAU WA TAKWIMU KUFUATA SHERIA NA TARATIBU ZA UTOAJI TAKWIMU
kiungo : NBS YAWATAKA WADAU WA TAKWIMU KUFUATA SHERIA NA TARATIBU ZA UTOAJI TAKWIMU
NBS YAWATAKA WADAU WA TAKWIMU KUFUATA SHERIA NA TARATIBU ZA UTOAJI TAKWIMU
Na Bushiri Matenda Na Agness Moshi - MAELEZO
Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania (NBS) imetoa rai kwa wadau wa Takwimu Nchini kufuata kanuni na taratibu za utoaji takwimu ili kuepusha sintofahamu baina yao, wapokeaji taarifa na Taasisi husika .
Rai hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa NBS Dkt. Albina Chuwa wakati akiongea na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam leo kufuatia taarifa zisizo sahihi zilizotolewa na Kampuni ya Utafiti ya Geopoll yenye ofisi ya Kanda ya Afrika, mjini Nairobi, Kenya kuhusiana Viwango na Idadi ya watazamaji wa vituo mbali mbali vya habari vinavyorushwa hapa nchini .
“Taarifa zozote zinazohusu utafiti ni lazima zihusishe wadau mbalimbali, na kwa kuzingatia vigezo vyote vinavyotakiwa na mamlaka iliyoidhinishwa kisheria kuhusiana na utoaji takwimu”, Dkt.Chuwa alivitaja vigezo hivyo kuwa ni pamoja na uwazi na ukweli, uhusishwaji wa Wadau na kwa kuzingatia weledi.
Aidha, amefafanua kuwa ni vyema Taasisi yoyote inayotaka kukusanya taarifa mbalimbali za takwimu ni budi kushirikisha wahusika ili kuepusha mkanganyiko na upotoshwaji kama ilivyofanywa na Kampuni hiyo kutoka Nairobi, Kenya.
“Takwimu zinazotolewa bila kuzingatia taratibu zinazohitajika hazitatambulika na Serikali kwani utoaji wa Takwimu haufanywi kama unavyohesabu migomba shambani, hivyo ni lazima wahusika wafuate taratibu zote”, alifafanua Dkt.Chuwa.
Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) ni Taasisi ya Umma iliyoanzishwa kwa Sheria ya Takwimu ya Mwaka 2015. Kwa mujibu wa Sheria hiyo, NBS imepewa mamlaka ya kutoa, kusimamia na kuratibu upatikanaji wa Takwimu rasmi kwa ajili ya matumizi ya Serikali na Wadau wa Takwimu.
Mkurugenzi mkuu Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani katika mkutano uliofanyika ukumbi wa Habari maelezo Jijini Dar es Salaam , kushoto Bw. Ephraim Kwisigabo Mkurugenzi Sensa na Takwimu za jamii.
Hivyo makala NBS YAWATAKA WADAU WA TAKWIMU KUFUATA SHERIA NA TARATIBU ZA UTOAJI TAKWIMU
yaani makala yote NBS YAWATAKA WADAU WA TAKWIMU KUFUATA SHERIA NA TARATIBU ZA UTOAJI TAKWIMU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala NBS YAWATAKA WADAU WA TAKWIMU KUFUATA SHERIA NA TARATIBU ZA UTOAJI TAKWIMU mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/08/nbs-yawataka-wadau-wa-takwimu-kufuata.html
0 Response to "NBS YAWATAKA WADAU WA TAKWIMU KUFUATA SHERIA NA TARATIBU ZA UTOAJI TAKWIMU"
Post a Comment