title : MWANAMUZIKII JAGUAR ASHINDA KITI CHA UBUNGE HUKO KENYA
kiungo : MWANAMUZIKII JAGUAR ASHINDA KITI CHA UBUNGE HUKO KENYA
MWANAMUZIKII JAGUAR ASHINDA KITI CHA UBUNGE HUKO KENYA
Msanii kutoka nchini Kenya, Charles Njagua a.k. Jaguar mara baada ya kushinda kiti cha ubunge katika jimbo la Starehe Nairobi, amesema kwake muziki bado unaendelea kwa sababu ndio umefanya watu kumjua.
“Nishaingia studio na sasa hivi nilikuwa naongea na prodyuza wangu tutaonana jioni, hivyo ninasema muziki unaendaelea na uongozi unaendelea, sitaacha kutunga nyimbo kwa sababu ndio imefanya watu kuweza kunijua na niendeleze vile vitu nimekuwa nikifanyia kwenye jamii,” ameiambia Mambo Mseto ya Radio Citizen na kuongeza.
“Kwanza kuna wasanii wengi wao walinisapoti na zile shida ambazo tumekuwa tukizipitia nitaenda kuzizungumza bungeni, kwa hiyo nitashirikiana na vijana wenzangu kuhakikisha wasanii na vijana wote mambo yao yanakuwa katika mpangilio,” amesema.
Alipoulizwa kama umaarufu wanaopata wasanii ndio unapelekea wengi wao kushinda pindi wanapogombea nyadhifa za uongozi, Jaguar alisema hilo halina ukweli bali ni namna msanii anavyokuwa karibu na jamii.
“Ni wasanii wengi wamegombea na wakashindwa, usanii pekee hauwezi kukusaidia kwa sababu hauendi bungeni kukatika useme Jaguar amechanguliwa akaimbe huko bungeni, naweza kusema ni vile unakuwa karibu na watu kwa sababu kuna wasanii wanakuwa wakubwa hawaonani na watu lakini kuna yule msanii anajulikana, anabarikiwa na Mungu lakini anarudi kukaa na watu,” amesema.
Hivyo makala MWANAMUZIKII JAGUAR ASHINDA KITI CHA UBUNGE HUKO KENYA
yaani makala yote MWANAMUZIKII JAGUAR ASHINDA KITI CHA UBUNGE HUKO KENYA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MWANAMUZIKII JAGUAR ASHINDA KITI CHA UBUNGE HUKO KENYA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/08/mwanamuzikii-jaguar-ashinda-kiti-cha.html
0 Response to "MWANAMUZIKII JAGUAR ASHINDA KITI CHA UBUNGE HUKO KENYA"
Post a Comment