Msafara wa DC washambuliwa na watu wasiojulikana

Msafara wa DC washambuliwa na watu wasiojulikana - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Msafara wa DC washambuliwa na watu wasiojulikana, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Msafara wa DC washambuliwa na watu wasiojulikana
kiungo : Msafara wa DC washambuliwa na watu wasiojulikana

soma pia


Msafara wa DC washambuliwa na watu wasiojulikana

Mkuu wa Wilaya ya  Karagwe, Godfrey Mheluka 

Karagwe. Msafara wa Mkuu wa Wilaya ya  Karagwe, Godfrey Mheluka uliokuwa katika operesheni ya kuwaondoa watu wanaodaiwa kuvamia maeneo ya wafugaji katika Kijiji cha Kashanda, Kata ya Nyakahanga, umeshambuliwa na watu wasiojulikana.

Katika shambulizi hilo lililotokea leo Agosti 29 saa tano asubuhi, diwani wa Nyakahanga, Charles Bechumila amejeruhiwa na amepelekwa katika Hospitali Teule ya Nyakahanga.

Mkuu wa wilaya hiyo, Mheluka amesema bado hajawa sawa, hivyo atazungumzia tukio hilo  baadaye.

Ofisa Tarafa ya Bugene Nyaishozi, Rozaria Christian amesema walikuwa kwenye operesheni halali na wakulima hawana na taarifa.

Amesema baada ya kuwakamata wawili ndipo kundi la watu lilijitokeza likionyesha kuwa lilijiandaa kuwashambulia.

Christian amesema watu kadhaa wamekamatwa wakituhumiwa kuhusika kumjeruhi diwani huyo.

Shuhuda wa tukio hilo aliyekuwa kwenye msafara huo amesema baada ya kufika kijijini humo aliwakuta baadhi ya watu wakilima na walikamatwa.

Baada ya kukamatwa amesema kundi hilo la watu liliwashambulia kwa mishale na mikuki hivyo walikimbia ndipo diwani alipojikwaa na kuanguka na watu hao wasiofahamika walimshambulia kwa  kumchoma mishale na kumkata kwa panga.


Hivyo makala Msafara wa DC washambuliwa na watu wasiojulikana

yaani makala yote Msafara wa DC washambuliwa na watu wasiojulikana Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Msafara wa DC washambuliwa na watu wasiojulikana mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/08/msafara-wa-dc-washambuliwa-na-watu.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Msafara wa DC washambuliwa na watu wasiojulikana"

Post a Comment