Mfanyabiashara Maarufu Zanzibar na Mwanamichezo Mhe Mohammrd Raza Amwaga Vifaa Vya Michezo na Zawadi Kwa Maskuli na Mikoa.

Mfanyabiashara Maarufu Zanzibar na Mwanamichezo Mhe Mohammrd Raza Amwaga Vifaa Vya Michezo na Zawadi Kwa Maskuli na Mikoa. - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Mfanyabiashara Maarufu Zanzibar na Mwanamichezo Mhe Mohammrd Raza Amwaga Vifaa Vya Michezo na Zawadi Kwa Maskuli na Mikoa., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Mfanyabiashara Maarufu Zanzibar na Mwanamichezo Mhe Mohammrd Raza Amwaga Vifaa Vya Michezo na Zawadi Kwa Maskuli na Mikoa.
kiungo : Mfanyabiashara Maarufu Zanzibar na Mwanamichezo Mhe Mohammrd Raza Amwaga Vifaa Vya Michezo na Zawadi Kwa Maskuli na Mikoa.

soma pia


Mfanyabiashara Maarufu Zanzibar na Mwanamichezo Mhe Mohammrd Raza Amwaga Vifaa Vya Michezo na Zawadi Kwa Maskuli na Mikoa.

Na Salum Vuai, Maelezo.
MKURUGENZI wa kampuni ya usafiri wa anga na huduma za viwanja vya ndege Zanzibar (ZAT) Mohammedraza Hassanali, ametoa wito kwa kampuni na taasisi mbalimbali kuunga mkono juhudi za serikali kuimarisha michezo maskulini.

Akizungungumza wakati wa hafla ya kukabidhi vitu mbalimbali kwa ajili ya zawadi za washindi kwenye mashindano ya mpira wa miguu mikoa ya Unguja na Pemba iliyofanyika nyumbani kwake Kibweni, Raza alisema ni wajibu wa kila Mzanzibari kusaidia sekta ya michezo.

Alifahamisha kuwa, iwapo wafanyabiashara wa Zanzibar wataunganisha nguvu kwa lengo la kuinua michezo kuanzia ngazi ya skuli ambako ndiko kwenye msingi wa vipaji vizuri, nchi hii itafika mbali kimichezo na kulitangaza vyema jina la Zanzibar.    

“Hii ninchi yetu sote, tuna wajibu kusaidia juhudi za serikali, na nimpongeze Mhe. Rais kwa kuteua Mkurugenzi makini na mwenye jitihada kuongoza Idara ya Michezo na Utamaduni,” alieleza Raza.

Raza ambaye pia ni Mwakilishi wa jimbo la Uzini, alisema hatachoka kutoa msukumo katika sekta ya michezo na misaada mingine ya kijamii, na vitu hivyo alivyotoa ni kutimiza ahadi yake aliyoitoa kabla mbele ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.

Katika hafla hiyo, Mkurugenzi huyo alikabidhi vityu mbalimbali kwa Mkurugenzi wa Uendeshaji na Utumishi kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Omar Ali Bai kwa ajili ya zawadi za washindi na washirikiwenmgine wa mashndano hayo yaliyopangwa kuanza Septemba 12, 2017 katika uwanja wa Amaan.

Mkurugenzi Bai aliyemuwakilisha Katibu Mkuu wa wizara yake Bi. Khadija Bakari Juma, akimshukuru Mhe. Raza, alisema kuwekeza katika michezo maskulini ni jambo muhimu kwa kuinua ufahamu wa wanafunzi masomoni.

Alisema dhana za watu wanaodhani mchezo inarejesha nyuma maendeleo ya masomo sio sahihi, kwani ushahidi duniani unaonesha wanafunzi wengine mahodari wamekuwa wakijikita kucheza michezo mbalimbali.

“Akili nzuri hutoka kwenye mwili wenye afya ambao kujengeka kwake kunatokana na mtu kujishughulisha katika michezo ambayo wataalamu wanasema ni sehemu bora kwa makuzi ya watoto”, alieleza.

Alimuahidi mfadhili huyo kwamba vitu vyote alivyovitoa vitafika kwa walengwa, huku akiwaomba wananchi wengine wenye uwezo, makampuni na wafanyabsiahara mbalimbali kushirikiana ili Zanzibar irejeshe hadhi yake michezoni ambayo kwa miaka ya karibuni imeonekana kutetereka.

Mapema, Mkurugenzi wa Idara ya Michezo na Utamaduni katika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali, alimshukuru Raza kwa moyo wake wa uzalendo, na kuwa tayari kutumia mali zake katika kujenga ustawi wa nchi.

Alisema kuwa Rais Dk. Shein amepania kwa dhati kuendeleza michezo kama anavyofanya katika mambo mengine, na akamsifu Raza kwa kuwa kiungo kizuri kati ya idara yake wanafunzi na watu wengine katika kuhakikisha michezo nchini inapiga hatua.         

Katika hafla hiyo, Raza alikabidhi kalkuleta za kisasa, madishi ya kuhifadhia chakula na kalamu huku akiahidi kufanya mambo mengine makubwa kwa ajili ya kuwashajiisha washiriki wa mashindano hayo ya mikoa sita ya Unguja na Pemba.

IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO
ZANZIBAR-22 AGOSTI, 2017.  


Hivyo makala Mfanyabiashara Maarufu Zanzibar na Mwanamichezo Mhe Mohammrd Raza Amwaga Vifaa Vya Michezo na Zawadi Kwa Maskuli na Mikoa.

yaani makala yote Mfanyabiashara Maarufu Zanzibar na Mwanamichezo Mhe Mohammrd Raza Amwaga Vifaa Vya Michezo na Zawadi Kwa Maskuli na Mikoa. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Mfanyabiashara Maarufu Zanzibar na Mwanamichezo Mhe Mohammrd Raza Amwaga Vifaa Vya Michezo na Zawadi Kwa Maskuli na Mikoa. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/08/mfanyabiashara-maarufu-zanzibar-na.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Mfanyabiashara Maarufu Zanzibar na Mwanamichezo Mhe Mohammrd Raza Amwaga Vifaa Vya Michezo na Zawadi Kwa Maskuli na Mikoa."

Post a Comment