title : MAKAMU WA RAIS MH.SAMIA SULUHU MGENI RASMI NANENANE
kiungo : MAKAMU WA RAIS MH.SAMIA SULUHU MGENI RASMI NANENANE
MAKAMU WA RAIS MH.SAMIA SULUHU MGENI RASMI NANENANE
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania, Mhe Samia, Suluhu Hassan leo anatarajiwa kuwaongoza Watanzania katika maadhimisho ya siku ya wakulima na Wafugaji nchini Tanzania ambapo kitaifa yatafanyika katika viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi.
Katika Kilele hicho cha Nane Nane Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu, atatembelea mabanda mbalimbali yakiwemo ya Kilimo, Ufugaji na Uvuvi yaliyopo katika viwanja hivyo ikiwa ni pamoja na kuhutubia wananchi na wakulima na Wafugaji watakaojitokeza katika maadhimisho hayo.
Makamu wa Rais aliwasili Mkoani Lindi jana kwa ajili ya sherehe hizo na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Lindi Godfrey Zambi, Viongozi mbalimbali wa serikali, Wanachama wa Chama cha Mapinduzi na vikundi vya ngoma ambavyo vilimlaki kwa nyimbo mbalimbali.
Licha ya Sherehe hizo Kilele chake Kitaifa kufanyika Mkoani Lindi kwa Kanda ya Kusini Lakini Nyanda za Juu Kusini yatafanyika katika viwanja vya viwanja vya John Mwakangale Mkoani Mbeya, Kanda ya kati ni Nzuguni Mkoani Mbeya, Kanda ya Kaskazini yatafanyika jijini Arusha na Kanda ya Mashariki yatafanyika mjini Morogoro.
Hivyo makala MAKAMU WA RAIS MH.SAMIA SULUHU MGENI RASMI NANENANE
yaani makala yote MAKAMU WA RAIS MH.SAMIA SULUHU MGENI RASMI NANENANE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MAKAMU WA RAIS MH.SAMIA SULUHU MGENI RASMI NANENANE mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/08/makamu-wa-rais-mhsamia-suluhu-mgeni.html
0 Response to "MAKAMU WA RAIS MH.SAMIA SULUHU MGENI RASMI NANENANE"
Post a Comment