title : KAMATI YA BUNGE KUTOKA MALAWI WAZURU MLIMA RUNGWE
kiungo : KAMATI YA BUNGE KUTOKA MALAWI WAZURU MLIMA RUNGWE
KAMATI YA BUNGE KUTOKA MALAWI WAZURU MLIMA RUNGWE
mwambawahabariBaadhi ya Wabunge wa Kamati ya Maliasili na Mabadiliko ya tabia ya nchi kutoka nchini Malawi wakiwa wanapanda jana Mlima Rungwe ambapo waliweza kupanda mlima huo mpaka kituo cha kwanza cha mapumziko
…………………………………………………………..
Wabunge wa Kamati ya Maliasili na Mabadiliko ya tabia ya nchi kutoka nchini Malawi wamefanya ziara ya mafunzo kwenye Msitu wa asili wa Hifadhi wa Mlima Rungwe mkoani Mbeya na kujionea jinsi wananchi wanavyoshirikishwa katika uhifadhi wa pamoja.
Akizungumza Mwenyekiti wa kamati hiyo, Welani Chilenga amesema lengo la ziara hiyo ni kutaka kujifunza jinsi Wakala wa Huduma Misitu Tanzania (TFS) wanavyofanya uhifadhi kwa kuwashirikisha wananchi katika kuzilinda hifadhi zao.
Amesema nchini Malawi wao wamekuwa wakitumia mitutu katika kulinda Misitu jambo ambalo halijawawezesha kufanikiwa katika uhifadhi hivyo sehemu kubwa ya miti yao imekatwa.
Chilenga amesema wamejionea vyanzo vya maji ambapo mlima huwa ni chanzo cha mito 21 na wameiomba TFS kuendelea na juhudi za uhifadhi kwani nao wamekuwa wakifaidika na Mlima huo kama chanzo chao cha maji kupitia ziwa Nyasa
Katika hatu nyingine, Wabunge wa Kamati hiyo walifanikiwa kupanda mlima huo mpaka kituo cha kwanza cha mapumziko.
Awali, Mhifadhi Mkuu wa Mlima Rungwe, Innocent Lupembe amewataka watanzania kutembelea hifadhi hiyo ili waweze vivutio mbalimbali vinavyopatikana katika hifadhi hiyo wakiwemo ndege na wanyama wa aina mbali mbali.
Aidha, Aliwataka watafiti wa ndani na nje ya nchi wafanye tafiti katika hifadhi hiyo kwa kuwa ina amali ambayo haipatikani mahali popote pale duniani nisipokwa katika Mlima huo.
Hivyo makala KAMATI YA BUNGE KUTOKA MALAWI WAZURU MLIMA RUNGWE
yaani makala yote KAMATI YA BUNGE KUTOKA MALAWI WAZURU MLIMA RUNGWE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala KAMATI YA BUNGE KUTOKA MALAWI WAZURU MLIMA RUNGWE mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/08/kamati-ya-bunge-kutoka-malawi-wazuru.html
0 Response to "KAMATI YA BUNGE KUTOKA MALAWI WAZURU MLIMA RUNGWE"
Post a Comment