Hazina yaibuka kidedea Wilaya ya Kinondoni.

Hazina yaibuka kidedea Wilaya ya Kinondoni. - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Hazina yaibuka kidedea Wilaya ya Kinondoni., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Hazina yaibuka kidedea Wilaya ya Kinondoni.
kiungo : Hazina yaibuka kidedea Wilaya ya Kinondoni.

soma pia


Hazina yaibuka kidedea Wilaya ya Kinondoni.

 Mthibiti ubora wa Shule Wilaya ya  Kinondon, Victoria Mollel, (katikati,) akikabidhi zawadi kwa mwanafunzi Perfect Mugisha wa Hazina aliyeongoza  kwenye mitihani ya majaribio iliyoandaliwa  na shule ya  Crown ya Mbezi Makonde Dar es salaam. Kushoto ni Mshauri wa shule ya sekondari ya Crown, Moses Kyando na kulia ni Mkurugenzi wa shule ya Crown Mary Shirima.

Na Mwandishi Wetu.
SHULE ya Msingi Hazina ya jijini Dar es Salaam, imefanikiwa kuwa ya kwanza kwa Wilaya ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam,  katika matokeo ya mitihani ya majaribio (Mock) ya darasa la saba kati ya shule 135.

Kwenye matokeo hayo yaliyotangazwa na Ofisa Elimu wa Wilaya Kinondoni, Kiduma Mageni yanaonyesha kuwa shule ya Hazina pia imefanikiwa kuingiza wanafunzi kumi bora kwa upande wa wavulana na kumi bora kwa upande wa wasichana.

Wavulana waliofanikiwa kuingia kumi bora ni Perfect Ndyetabula,, Abdurahim Sagin, Hamza Almas, Maxmbwana Max, Phinny Murungu, Walter Kiunsi na Hafidh Mohamed, Derick Ignas Menelick Sanga na Brighton Lyatuu.

Kwa upande wa wasichana waliofanya vizuri aliwataja kuwa ni Abeer Ally, Chipwe Ramson, Florensiana Simon, Ashine Mohamed, Cherish Narcis, Safina Mzuanda, Sandra lema, Evoduia Mayombo, Leyla Sagin, Najra Kimaro na Shufaa Juma.

 Akizungumzia siri ya mafanikio ya shule yake, Mwalimu Mkuu wa shule hiyo,  Patrick Cheche, alisema kujituma kwa walimu na ushurikiano ambao wamekuwa wakiupata kwa uongozi wa shule na wanafunzi ndiyo kitu wanachojivunia.

“Walimu wanafanyakazi kwa moyo sana, wazazi wa wanafunzi wamekuwa wakitoa ushirikiano mzuri sana kwa shule na uongozi wa shule unawajali sana walimu, hayo kwa pamoja yamekuwa yakisaidia ufaulu wetu kuwa juu mwaka hadi mwaka,” alisema Mwalimu Patrick

Aliwapongeza wanafunzi kwa mafanikio hayo na kuwataka wasome kwa bidii ili hatimaye waweze kuongoza kitaifa na  Mkoa wa Dar es Salaam kwenye mitihani ya darasa la saba mwaka huu.


Hivyo makala Hazina yaibuka kidedea Wilaya ya Kinondoni.

yaani makala yote Hazina yaibuka kidedea Wilaya ya Kinondoni. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Hazina yaibuka kidedea Wilaya ya Kinondoni. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/08/hazina-yaibuka-kidedea-wilaya-ya.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Hazina yaibuka kidedea Wilaya ya Kinondoni."

Post a Comment