title : JUNDOKAN TANZANIA - GOJU RYU KARATE-DO” KUPANDISHA NGAZI WANAFUNZI WA DOJO DAR
kiungo : JUNDOKAN TANZANIA - GOJU RYU KARATE-DO” KUPANDISHA NGAZI WANAFUNZI WA DOJO DAR
JUNDOKAN TANZANIA - GOJU RYU KARATE-DO” KUPANDISHA NGAZI WANAFUNZI WA DOJO DAR
Tunatarajia kufanya mitihani ya mikanda mieusi miezi ijayo madaraja tofauti kupitia dojo za “ Kaizen dojo” Jamhuri na dojo dada ya Hekalu la Kujilinda Zanaki dojo. Hii ni moja ya jitihada za kusambaza mwenendo huu kwa kina na pia ufundishaji wa mbinu za utumiaji wa tafsiri za “Kata” uijulikanao kama “Bunkai”, au uchambuzi wa matumizi ya mbinu za kujilinda. Mitihani yote itafanywa na sensei Rumadha Fundi chini ya utaratibu wa “Syllabus” ya Jundokan, Okinawa.
Pia wakati huohuo, kutakuwa na semina ya wanafunzi wa ngazi za mikanda mieusi wa Jundokan Tanzania ikiwemo na dojo ya Zanaki katika kuwawezesha wanafunzi wake kuuliza na kupata majibu ya matumizi yao ya ufanyaji Kata kama jinsi ipasavyo chini ya chama hicho chenye ufahasa wa mtindo huo unaofuata nyanyo za mafunzo ya Master Chojun Miyagi, mwanzilishi wa mtindo wa Okinawa Goju Ryu.
Pia vilevile, Tanzania imepatiwa mwaliko wa kuhudhuria maadhimisho ya miaka 65 tokea kuanzishwa kwa chama cha Jundokan itayofanyika November 2018 mjini Naha, Okinawa, Japan. Chama hicho kilianzishwa na mwanafunzi mkuu wa Master Miyagi aitwae Master Eiichi Miyazato sensei 1957 ambae pia alikuwa ndio mwalimu wa sensei Nantambu C Bomani. “ Chuo kinacho fundisha nyayo au mwenendo wa Master Chojun Miyagi”. Ikimaanisha, hamna mabadiliko yeyote kimafunzo na Kata zake kama jinsi alivyokuwa akifundisha mwanzilishi wake Chojun Miyagi sensei.
Hivyo makala JUNDOKAN TANZANIA - GOJU RYU KARATE-DO” KUPANDISHA NGAZI WANAFUNZI WA DOJO DAR
yaani makala yote JUNDOKAN TANZANIA - GOJU RYU KARATE-DO” KUPANDISHA NGAZI WANAFUNZI WA DOJO DAR Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala JUNDOKAN TANZANIA - GOJU RYU KARATE-DO” KUPANDISHA NGAZI WANAFUNZI WA DOJO DAR mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/08/jundokan-tanzania-goju-ryu-karate-do.html
0 Response to "JUNDOKAN TANZANIA - GOJU RYU KARATE-DO” KUPANDISHA NGAZI WANAFUNZI WA DOJO DAR"
Post a Comment