title : Waziri Prof. Mbarawa akagua mradi wa barabara za juu TAZARA jijini Dar es salaam
kiungo : Waziri Prof. Mbarawa akagua mradi wa barabara za juu TAZARA jijini Dar es salaam
Waziri Prof. Mbarawa akagua mradi wa barabara za juu TAZARA jijini Dar es salaam
Na Joachim Mushi wa TBN
WAZIRI wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa leo ametembelea mradi wa ujenzi wa barabara za juu unaoendelea eneo la Tazara jijini Dar es Salaam na kuridhishwa na kasi ya ujenzi inayoendelea chini ya Kampuni ya Sumitomo Mitsui Construction Co. Ltd ya nchini Japan.
Akizungumza katika ziara hiyo alisema lengo ni kuangalia maendeleo ya ujenzi wa mradi huo ili kuhakikisha unakamilika mapema kama ulivyopangwa. Prof. Mbarawa alisema ameridhishwa na maendeleo ya mradi huo ambao mara baada ya kukamilika utarahisisha shughuli za usafiri kwa wananchi watumiao barabara hizo mbili za Nyerere na Mandela jijini Dar es Salaam.
Mradi huo wa ujenzi unatarajiwa kukamilika ifikapo Oktoba 2018 huku ukitarajiwa kugharimu takribani shilingi bilioni 100, ambapo kati ya fedha hizo shilingi bilioni 93.44 zitatolewa na Japan kupitia Shirika la Ushirikiano wa Kimataifa (JICA), na Serikali ya Tanzania itatoa shilingi Bilioni 8.3.
Hivyo makala Waziri Prof. Mbarawa akagua mradi wa barabara za juu TAZARA jijini Dar es salaam
yaani makala yote Waziri Prof. Mbarawa akagua mradi wa barabara za juu TAZARA jijini Dar es salaam Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Waziri Prof. Mbarawa akagua mradi wa barabara za juu TAZARA jijini Dar es salaam mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/07/waziri-prof-mbarawa-akagua-mradi-wa.html
0 Response to "Waziri Prof. Mbarawa akagua mradi wa barabara za juu TAZARA jijini Dar es salaam"
Post a Comment