title : Wahitimu waliosoma China waombwa kuisaidia Tanzania katika uchumi wa viwanda
kiungo : Wahitimu waliosoma China waombwa kuisaidia Tanzania katika uchumi wa viwanda
Wahitimu waliosoma China waombwa kuisaidia Tanzania katika uchumi wa viwanda
WAZIRI wa Mambo ya Nje, Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Balozi Augustine Mahiga amesema wanafunzi wahitimu kutoka vyo vya nje ya nchi waunde umoja wa mataifa waliyotoka ili kuwa na jukwaa la kuvuna wataalamu pamoja na wao kutambuana.
Alisema hayo mwishoni mwa wiki wakati akizindua Chama cha wanafunzi waliosoma China (CAAT), jijini hapa ambapo alibainisha vyama vingi vya aina hiyo vimeanzishwa na kupotea kutokana na kukosa msukumo kutoka serikalini.
“Nyinyi mtakua kiungo kati ya wasomi kutoka China, serikali na jamii, hiki ni chama cha kwanza cha wanafunzi waliosoma China. Matarajio yangu ari iliyowafanya kujipanga pamoja itabaki daima na naamini chama hiki kitakua jukwaa la wanafunzi wanaoendelea kusoma na waliohitimu,” alisema Balozi Mahiga.
Aliongeza kuwa: “Najua kuna Wachina nchini walioanzisha viwanda na wangependa kupata vijana wasomi, hii ni fursa pekee ya kuendeleza sekta binafsi na kudumisha urafiki wetu. Ningeshauri idara za serikali na sekta binafsi kuwa karibu na chama hiki.
“Nimezungumza nao na nimeona aina ya utaalamu waliokuwa nao, utaalamu huu utasaidia kuleta tija kwa idara mbalimbali na wizara pamoja na taasisi za umma. Nitaangalia namna wizara yangu itakavyokisaidia chama hiki ili tusiwaache peke yao ubunifu waliofanya ni wa ahali ya juu kabisa.”
Balozi msaidizi wa China nchini, Bw.
Waziri wa Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki , Kikanda na Kimataifa Mhe, Dkt, Augustine Mahiga Wa kwanza (kushoto) ni Balozi msaidizi wa China Bwana. Gao Haudong wa pili (kulia) ni Balozi wa Tanzania Nchini China Bwana. Mbelwa Kairuki wakinena jambo kwenye hafla fupi ya kuzinduzi wa Ofisi za umoja wa wahitimu Wanafunzi Watanzania walio Soma nchini China au China Alumni Association of Tanzania(CAAT) iliyofanyika
jijini Dar es salaam.
Waziri wa Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki , Kikanda na Kimataifa Mhe, Dkt, Augustine akinena jambo na Balozi msaidizi wa China Bwana. Gao Haudong kwenye hafla fupi ya kuzindua Chama cha umoja wa wahitimu, Wanafunzi Watanzania walio Soma Nchini China (CAAT) jijini Dar es salaam.
Waziri wa Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki , Kikanda na Kimataifa Mhe, Dkt, Augustine akiambatana na Balozi msaidizi wa China Bwana. Gao Haudong kwenye uzinduzi wa ofisi za umoja wa wahitimu, Wanafunzi Watanzania walio Soma Nchini China (CAAT) ) iliyo fanyika Posta jijini Dar es salaam.
Waziri wa Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Kikanda na Kimataifa Mhe, Dkt, Augustine Katikati akipata picha ya pamoja na wanaumoja wa (CAAT) wapili (kulia) ni Balozi wa Tanzania Nchini China Bwas. Mbelwa Kairuki wa kwanza (kushoto) ni Mwenyekiti wa (CAAT) DKT.Liggy Vumilia wa pili (kushoto) ni Balozi msaidizi wa China Bwana. Gao Haudong kwenye hafla fupi ya kuzindua Ofisi za Chama wa wahitimu, Wanafunzi Watanzania walio Soma Nchini China (CAAT) iliyo fanyika jijini Dar es salaam. Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA
Hivyo makala Wahitimu waliosoma China waombwa kuisaidia Tanzania katika uchumi wa viwanda
yaani makala yote Wahitimu waliosoma China waombwa kuisaidia Tanzania katika uchumi wa viwanda Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Wahitimu waliosoma China waombwa kuisaidia Tanzania katika uchumi wa viwanda mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/07/wahitimu-waliosoma-china-waombwa.html
0 Response to "Wahitimu waliosoma China waombwa kuisaidia Tanzania katika uchumi wa viwanda"
Post a Comment