Utalii Wetu : Utalii Wazidi Kuongezea Pato la Taifa

Utalii Wetu : Utalii Wazidi Kuongezea Pato la Taifa - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Utalii Wetu : Utalii Wazidi Kuongezea Pato la Taifa, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Utalii Wetu : Utalii Wazidi Kuongezea Pato la Taifa
kiungo : Utalii Wetu : Utalii Wazidi Kuongezea Pato la Taifa

soma pia


Utalii Wetu : Utalii Wazidi Kuongezea Pato la Taifa


Na Thobias Robert-Maelezo
Sekta ya utalii nchini imeendelea kukuza na kuongeza mapato ya serikali kwa kuchangia zaidi ya asilimia 17 ya pato la taifa, huku ikitazamiwa kuongezeka katika mwaka huu wa fedha.

Hayo yalisemwa Jana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za taifa (TANAPA) Bwana Allan Kijazi wakati akizungumza katika kipindi cha TUNATEKELEZA” kinachorushwa na Televisheni ya Taifa (TBC1).
“Utalii unatoa mchango mkubwa sana katika uchumi wa nchi hii, kwa sasa hivi unakisiwa kwamba unachangia kama asilimia 17.2 ya pato la taifa na asilimia 25 ya fedha ya kigeni,” alisema Bw. Kijazi. huku akisisitiza kuwa TANAPA watazidi kulinda na kuendeleza hifadhi zilizopo nchini ili zizidi kuongeza pato la taifa kwa maendeleo ya watanzania wote.
Mkurugenzi huyo wa TANAPA alisema kuwa katika mwaka wa fedha 2016/2017 TANAPA ilichangia kiasi cha billion 27 kwenda Mfuko wa Taifa wa serikali na matarajio yao katika kuchangia mfuko wa fedha wa Taifa kwa mwaka huu wa fedha 2017/2018 ni bilioni 33.4 hii ni kwa sababu ya kuongezeka kwa Watalii kutoka nje ya nchi.
Aliongeza kuwa Tanzania ina vivutio vingi kama vile Mito, Mabonde, Milima, lakini hifadhi za Taifa kama Vile Ngorongoro, Serengeti, Gombe, Ruaha ndizo zinazoongoza kwa kuchangia pato la taifa kwa zaidi ya asilimia 80 ikilinganishwa na vivutio vingine.
Bwana Kijazi aliongeza kwa kusema kuwa, utalii nchini umekuwa ukikuunaongezeka kila mwaka ambapo kwa takimwu walizo nazo zinaonesha kuwa, ongezeko la watalii kwa miaka mitano iliyopita limekuwa lilkiongezeka kwa asilimia 4 hadi 7 kila mwaka.
Kuongeza kwa watalii hasa katika hifadhi za Taifa kunatokana na TANAPA kujitangaza zaidi katika nchi mbalimbali duniani kupitia Mitandao ya kijamii, Makampuni binafsi ndani na nje ya nchi, Balozi za Tanzania katika mataifa ya Nje, Vilabu mbalimbali vya Ulaya na Amerika pamoja Vyombo vya Habari vya kimataifa kama vile CNN na BBC.
Mkurugenzi Kijazi alisema kuwa, Mataifa yanayoongoza kutembelea hifadhi za taifa ni pamoja na Marekani, Ujerumani, Uingereza, Italia, Ufaransa, pamoja na Hispania huku akitaja kuwa vivutio vya utalii vilivyopo Nchini hasa hifadhi ni vya kipekee, mazingira mazuri, hali ya hewa pamoja na amani na utulivu uliopo nchini ndiyo sababu zinazowavutia watalii kuongezeka kila mwaka.
Pamoja na kukua na kuongezeka kwa utalii nchini kunakopelekea kuongeza la Taifa, Mkurugenzi Kijazi alisema kuwa, utalii wa ndani bado ni changamoto kwani watalii wengi wanatoka nje ya Nchi huku wazawa wakishindwa kuzuru maeneo mbalimbali ya utalii ili kujionea fahari ya nchi yao hivyo ametoa wito kwa Watanzania kutembelea vivutio hivyo ili kukuza na kuongeza pato la Taifa.

Hivi karibuni Mtandao wa SafariBookings.com unaojihusisha na masuala ya ukuzaji wa safari za kitalii barani Afrika uliitaja Tanzania kama kivutio kizuri cha safari za watalii barani humu.


Hivyo makala Utalii Wetu : Utalii Wazidi Kuongezea Pato la Taifa

yaani makala yote Utalii Wetu : Utalii Wazidi Kuongezea Pato la Taifa Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Utalii Wetu : Utalii Wazidi Kuongezea Pato la Taifa mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/07/utalii-wetu-utalii-wazidi-kuongezea.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Utalii Wetu : Utalii Wazidi Kuongezea Pato la Taifa"

Post a Comment