title : Taswa FC yachapwa mabao 3-2 na TPB bank FC
kiungo : Taswa FC yachapwa mabao 3-2 na TPB bank FC
Taswa FC yachapwa mabao 3-2 na TPB bank FC
Timu ya soka ya TPB Bank FC imefanikiwa kulipiza kisasi kwa timu ya waandishi wa habari za michezo nchini, Taswa FC baada ya kuifunga kwa mabao 3-2 katika mchezo huo maalum uliofanyika kwenye uwanja wa Shule ya Sheria (Law School) uliopo maeneo ya kituo cha mabasi cha Mawasiliano jijini Dar es salaam.
Katika mchezo wa kwanza, Taswa FC iliifunga TPB Bank FC kwa mabao 4-0 katika mchezo uliofanyika kwenye uwanja huo huo.
TPB Bank FC ilitumia idadi pungufu ya wachezaji wa Taswa FC kufunga mabao yote katika mchezo huo ambao pia ulikuwa wa maandalizi kwa timu hiyo ya benki kuelekea katika mashindano ya soka ya taasisi za kibenki yanayotarajiwa kuanza hivi karibuni. Taswa FC ilianza mechi hiyo ikiwa na wachezaji nane tu.
Bao la kwanza la TPB Bank FC lilifungwa na nahodha wa timu hiyo, Baraka Kyomo katika dakika ya 10 ya mchezo baada ya kuwashinda kasi mabeki wa Taswa FC na kufunga kirahisi.
Wakati Taswa FC ikijiuliza, Kyomo alifunga bao la pili katika dakika ya 17 kabla ya Ojo Ajali kufunga la tatu katika dakika ya 35 ya mchezo.
Taswa FC ilianza harakati za kusawazisha mabao hayo kuanzia kipindi cha pili baada ya kutimia wachezaji wote 11. Bao la kwanza la Taswa FC lilifungwa na Fred Pastory baada ya kupokea pasi safi ya Zahoro Mlanzi kabla ya Shedrack Kilasi kufunga la pili kufutia mpira wa kona wa Juma Ramadhani.
Kiongozi wa timu hiyo Chichi Banda alisema kuwa wamefuraishwa na ushindi huo na kuwaomba Taswa FC kujipanga kwa ajili ya mchezo unaofuata
TPB bank FC
Taswa FC
Hivyo makala Taswa FC yachapwa mabao 3-2 na TPB bank FC
yaani makala yote Taswa FC yachapwa mabao 3-2 na TPB bank FC Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Taswa FC yachapwa mabao 3-2 na TPB bank FC mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/07/taswa-fc-yachapwa-mabao-3-2-na-tpb-bank.html
0 Response to "Taswa FC yachapwa mabao 3-2 na TPB bank FC"
Post a Comment