SERIKALI HAIJAFUTA MAFUNZO KWA WATUMISHI WA UMMA

SERIKALI HAIJAFUTA MAFUNZO KWA WATUMISHI WA UMMA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa SERIKALI HAIJAFUTA MAFUNZO KWA WATUMISHI WA UMMA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : SERIKALI HAIJAFUTA MAFUNZO KWA WATUMISHI WA UMMA
kiungo : SERIKALI HAIJAFUTA MAFUNZO KWA WATUMISHI WA UMMA

soma pia


SERIKALI HAIJAFUTA MAFUNZO KWA WATUMISHI WA UMMA

Serikali haijafuta mafunzo kwa watumishi wa umma ambapo Taasisi za Serikali zimeelekezwa kuandaa Mpango wa Mafunzo kwa watumishi kwa njia ya uwazi na shirikishi ili kuepuka malalamiko kutoka kwa baadhi ya watumishi wa umma.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) amesema hayo leo katika kikao kazi na Watumishi wa Umma wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, jijini Dar es Salaam.

Mhe. Kairuki amesema mwajiri anapoandaa Mpango wa Mafunzo kwa watumishi wake ni vyema mpango huo ukawa shirikisha kwa watumishi wote ili kujua mpangilio wake, ikiwa ni pamoja na kuandaa orodha ya ziada ya watumishi watakaochukua nafasi za wale waliopangwa kushiriki mafunzo lakini wakashindwa.

“Napokea malalamiko mengi sana kuhusiana na upendeleo katika suala la mafunzo, napenda kuwasisitiza waajiri tuandae Mpango wa Mafunzo ambao ni shirikishi kwa watumishi wote kuepuka haya, wengine wanapangwa na hawashiriki mafunzo,” Mhe. Kairuki amesema na kuongeza baadhi ya watumishi wa umma wanapangwa kushiriki mafunzo na hawaendi kwa sababu mbalimbali, lakini fursa ya nafasi hizo hawapangiwi wengine ili kuendana na mpango.

Mhe. Kairuki ameongeza kuwa Mpango wa Mafunzo shirikishi pamoja na kuondoa malalamiko, utasaidia pia kutorudisha fedha zilizobaki kwa watumishi wa umma ambao walipangwa lakini wakashindwa kuhudhuria mafunzo kwa sababu mbalimbali.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akizungumza na viongozi na watumishi wa umma wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala alipofanya ziara ya kikazi  katika Manispaa hiyo ili kupokea maoni, ushauri na kusikiliza kero za watumishi wa umma leo Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mhe. Sophia Mjema akitoa hotuba ya kumkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) kuzungumza na watumishi wa umma katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilala wakati wa kikao kazi kilichofanyika katika Manispaa hiyo Jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Bw, Msongela Palela akiwasilisha taarifa ya manispaa anayoiongoza kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) alipofanya ziara ya kikazi katika Manispaa hiyo ili kupokea maoni, ushauri na kusikiliza kero za watumishi wa umma leo Jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya watumishi wa umma wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) (Hayupo pichani) wakati wa kikao kazi kilichofanyika leo Jijini Dar es Salaam.

Mthibiti Mkuu Ubora wa Shule – Manispaa ya Ilala, Bi. Juliana Mhonyiwa akiwasilisha hoja wakati wa kikao kazi kilichowakutanisha watumishi wa umma Halmashauri ya Manispaa ya Ilala na  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) leo Jijini Dar es Salaam.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA



Hivyo makala SERIKALI HAIJAFUTA MAFUNZO KWA WATUMISHI WA UMMA

yaani makala yote SERIKALI HAIJAFUTA MAFUNZO KWA WATUMISHI WA UMMA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala SERIKALI HAIJAFUTA MAFUNZO KWA WATUMISHI WA UMMA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/07/serikali-haijafuta-mafunzo-kwa.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "SERIKALI HAIJAFUTA MAFUNZO KWA WATUMISHI WA UMMA"

Post a Comment