title : RC Makonda alitembelea hospitali ya Amana, akagua jengojipya la Mama na Mtoto
kiungo : RC Makonda alitembelea hospitali ya Amana, akagua jengojipya la Mama na Mtoto
RC Makonda alitembelea hospitali ya Amana, akagua jengojipya la Mama na Mtoto
Paul Makonda .
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam akielezea juu ujenzi huo mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani).picha na mwambawa habari )
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam akielezea juu ujenzi huo mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani).picha na mwambawa habari )
Serikali ya Tanzania kupitia ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam imetembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa wodi ya kisasa ya kinamama na watoto inayoendelea kujengwa Hospital ya rufaa ya Amana yenye thamani ya shilingi Billion 1.2 ambapo ujenzi huo umekamilika kwa 100%.
Jitihada hizo zimefanywa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ambae kwa kiasi kikubwa amekuwa chachu ya maendeleo makubwa katika sekta ya afya katika mkoa wake.
Ikumbukwe tu katika jitihada za maendeleo ya idara ya afya zinazofanywa na mkuu huyo, ambapo tarehe 11 mwezi Julai mwaka huu alizindua jiwe la msingi la ujenzi wa jengo la huduma za dharula katika hospitali ya Temeke ikiwa ni mwendelezo wa kuhakikisha mkoa huo unaondokana na matatizo ama changamoto za afya.
Awali hospitali ya Mwananyamala ,na Amana zilikuwa na malalamiko mengi ikwemo wagonjwa kudai kutopata huduma ya uhakika, lakini Mkuu wa mkoa huyo amewatoa hofu wananchi wa mkoa wa Dar es salaam kuwa wao kama serikali wanaendeleza jitihada ya kuhakikisha mazingira ya utoaji huduma za afya katika hospitali hizo zinaimarika kwa kiasi kikubwa.
Huu ni muonekano wa jengo la zamani la kutolea huduma za akina mama na watoto. |
Wodi hiyo ya kisasa itakuwa na uwezo wa kuchukuwa vitanda 150 sambamba na Vifaa kisasa vya kutolea huduma, Vyumba vya Madaktari,vyoo vya kisasa,mabomba ya maji, taa za kisasa na sehemu ya kutosha ya wagonjwa kukaa wakati wakisubiri kuhudumiwa.
Ujenzi huo unafadhiliwa na Kampuni tanzu ya Mafuta na Saruji ya Amsons Group ambayo imekubali kumuunga mkono Mheshimiwa Makonda kwa kujenga wodi tatu wazazi na watoto kwenye Hospital za Amana, Temeke na Mwananyamala ambapo zote zitakuwa na uwezo wa kuchukuwa vitanda 450.
Muonekano wa jengo jipya la kutolea huduma za akina mama na watoto katika hospitali ya rufaa ya amana jiji Dar es salaam.
“Ujenzi huu na hatua iliyofikia inatoa matumaini mapya kwa kinamama, watoto na wakazi wa Dar es salaam juu ya upatikanaji wa huduma bora na nzuri kwenye Hospital zetu za Serikali,watu walishazoea huduma nzuri zinapatikana nje ya Hospital za Serikali lakini kwa sasa hali itabadilika, na nina uhakika ndani ya muda mfupi tutamuomba Rais Dr.Magufuli aje atuzindulie hizi wodi kama ishara ya kumbukumbu ya kazi aliyoianza alipotembelea Hospital ya Muhimbili na kukuta watu wamelala chini na kutafuta majibu, sisi wasaidizi wake ametupa kazi ya kutatua kero za wananchi, hivi ndivyo tunavyozitatua kwa vitendo” Alisema.
Aidha Makonda amesema wodi hiyo itazidisha upatikanaji mzuri wa huduma bora za Afya kwa wakazi wa jiji la Dar es salaam huku akieleza kuwa lengo lake ni kuhakikisha Dar es Salaam inakuwa mkoa unaotoa huduma bora za Afya.
“Kama mnakumbuka wakati tunakuja wodi iliyokuwa ikitumik akinamama walikuwa wakilundikana chini na wengine wanatumia kitanda kimoja zaidi ya watatu hadi wanne na wakati mwingine walikuwa wakilazimika kurudi nyumbani kabla ya muda wa madaktari kuruhusu kutokana na mazingira duni yaliyokuwa yakikabili wodi hiyo, lakini wodi hii itamaliza kero hiyo” Aliongeza Makonda.
Mkuu wa mkoa Dar e salaam Paul Makonda (wapili kushoto) akizungumza na Baadhi ya wauguzi wa hospitali ya rufaa ya amana. |
Hata hivyo Makonda amewataka wadau wa maendeleo wenye dhamira ya kuchangia shughuli za Maendeleo kwenye Mkoa wa Dar es salaam kujitokeza kwa wingi Ofisini kwake na Ofisi za Wilaya kuungana na Serikali kuujenga Mkoa huo.
“Nawapongeza watumishi na wafanyakazi wa Afya kwenye Hospital za Amana, Temeke na Mwananyamala kwa kazi kubwa wanayoifanya kupunguza kero kwenye Sekta ya Afya” Alisema Makonda.
Hivyo makala RC Makonda alitembelea hospitali ya Amana, akagua jengojipya la Mama na Mtoto
yaani makala yote RC Makonda alitembelea hospitali ya Amana, akagua jengojipya la Mama na Mtoto Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala RC Makonda alitembelea hospitali ya Amana, akagua jengojipya la Mama na Mtoto mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/07/rc-makonda-alitembelea-hospitali-ya.html
0 Response to "RC Makonda alitembelea hospitali ya Amana, akagua jengojipya la Mama na Mtoto"
Post a Comment