title : Mama Salma Kikwete awasisitiza wanamichezo pindipo wakihojiwa wajibu kwa kiswahili
kiungo : Mama Salma Kikwete awasisitiza wanamichezo pindipo wakihojiwa wajibu kwa kiswahili
Mama Salma Kikwete awasisitiza wanamichezo pindipo wakihojiwa wajibu kwa kiswahili
Na: Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.
Mama Salma ambae ni Balozi wa Kiswahili katika bara la Afrika ameyasema hayo asubuhi ya leo katika hafla maalum ya uzinduzi wa Makavazi na Jumuiya ya Watetezi wa Kiswahili Tanzania (WAKITA) iliyofanyika katika Ukumbi wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) huko Vuga Mjini Zanzibar.
Mama Salma amesema tamko la Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Tanzania Dkt Harrison George Mwakyembe la kuwataka wachezaji wanapohojiwa wajibu kwa Kiswahili yeye amefurahi sana kwani huo ni uzalendo na njia moja ya kukuza Kiswahili.
“Nakumbuka hata juzi tu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo DK Harrison Mwakyembe alitoa tamko muhimu wakati anawapokea wachezaji wa timu ya Taifa wa mpira wa miguu, aliwataka wachezaji wote wanapohojiwa na Waandishi wa Habari wa ndani na nje ya nchi wawe wanajibu kwa lugha ya Kiswahili, tamko hili mimi nimelifurahia kwa kuwa limeweza kukuza na kuitangaza lugha yetu ya Kiwahili ndani na nje ya nchi”. Alisema Mama Salma.
Mwanzoni mwa mwezi huu wa July, 2017 kuliibuka mjadala kwa baadhi ya wapenzi wa soka nchini Tanzania baada ya Mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Tanzania Elias Maguli kujibu kwa Kiswahili alipoulizwa swali kwa Kiengera na kituo kimoja cha TV huko Afrika ya Kusini baada ya kuibuka kuwa nyota wa mchezo kufuatia kufunga bao katika dakika ya 18 ya mchezo ambapo Stars waliichapa Afrika Kusini bao 1-0 katika Mashindano ya COSAFA CUP.
“Ahsante sana namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutuaajilia kuweza kupata ushindi katika mchezo huu. Ulikuwa mchezo muhimu sana ila tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujaalia kuweza kutoka na ushindi nawashukuru mashabiki waliojitokeza na kuweza kutushangilia na kutupatia nguvu”. Alisema Elius Maguli ambaye alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mchezo huo.
Hivyo makala Mama Salma Kikwete awasisitiza wanamichezo pindipo wakihojiwa wajibu kwa kiswahili
yaani makala yote Mama Salma Kikwete awasisitiza wanamichezo pindipo wakihojiwa wajibu kwa kiswahili Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Mama Salma Kikwete awasisitiza wanamichezo pindipo wakihojiwa wajibu kwa kiswahili mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/07/mama-salma-kikwete-awasisitiza.html
0 Response to "Mama Salma Kikwete awasisitiza wanamichezo pindipo wakihojiwa wajibu kwa kiswahili"
Post a Comment