title : MAKONDA ATEMBELEA GEREJI INAYOTENGENEZA MAGARI YA POLISI DAR ES SALAAM YALIYOPELEKWA KUTENGENEZWA.
kiungo : MAKONDA ATEMBELEA GEREJI INAYOTENGENEZA MAGARI YA POLISI DAR ES SALAAM YALIYOPELEKWA KUTENGENEZWA.
MAKONDA ATEMBELEA GEREJI INAYOTENGENEZA MAGARI YA POLISI DAR ES SALAAM YALIYOPELEKWA KUTENGENEZWA.
Mkuu wa Mkoa wa Mkoa wa Dar es salaam Mheshimiwa Paul Makonda leo ametembelea Garage ya utengenezaji wa Magari ya RSA Limited Mkoani Kilimanjaro kukagua maendeleo ya ukarabati na ubadilishaji mwonekano wa Magari mabovu 26 ya Jeshi la Polisi yaliyosafirishwa kwenda Moshi Mkoani Kilimanjaro hivi karibuni.
Akiwa katika Garage hiyo Mheshimiwa Makonda amejionea magari hayo yakiwa katika hatua mbalimbali za utengenezaji ambapo ameomba uongozi wa kampuni hiyo kukamilisha ukarabati wa magari hayo kwa wakati iliyaweze kuongezea ulinzi na usalama jijini Dar es salaam.
Aidha Makonda amesema kuwa anataka kubadili mwonekano wa jeshi la polisi Mkoa wa Dar es salaam kwa kuhakikisha magari ya polisi yanakuwa na hali nzuri itakayowawezesha kutekeleza majukumu yao kwa uufanisi kwa kuyabadili magari hayo kuwa kama yale ya Askari wa umoja wa mataifa.
*”Hakuna kitu kinachoninyima usingizi kama pale Mwananchi anapohitaji polisi wafike mahala pa tukio na polisi hawafiki, na kufanya hali ya amani kutoweka na wakati huohuo polisi wanataka kufanya kazi yao ila wanashindwa kutokana na uhaba wa vifaa.Hii ndiyo sababu ninahangaika ili siku moja Dar es Salam iwe na amani hata kufikia hatua ya watu kufanya Biashara zao masaa 24na kutembea kwa amani muda wote.”*alisema Makonda.
*Nimepata Pikipiki 200, baiskeli 500 na kuweza kutengeneza magari haya 56 kuwa na viwango vya kimataifa kama magari ya Umoja wa Mataifa (U.N) yanavyoonekana,yaani kwenye gari ya doria itaweza kuwa na maafisa wa polisi tisa kwa nyuma,ambao watatu watakuwa kushoto na watatu kulia mwa gari hiyo huku wawili wakiwa nyuma ya gari hiyo na mmoja akiwa amesimama mbele na silaha kubwa.”*aliiongeza Makonda.
Mkuu wa mkoa wa DEar es salaam Mh. Paul Makonda akikagua moja ya magari 26 ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Dar es salaam yaliyopelekwa katika Garage ya utengenezaji wa Magari ya RSA Limited Mkoani Kilimanjaro kwa ukarabati ili yaendane na kazi ya jeshi la p0lisi
Mkuu wa mkoa wa DEar es salaam Mh. Paul Makonda akijadiliana jamabo na uongozi wa Garage ya utengenezaji wa Magari ya RSA Limited Mkoani Kilimanjaro wakati alipokagua magari ya polisi yanayofanyiwa ukarabati mkubwa.
Mkuu wa mkoa wa DEar es salaam Mh. Paul Makonda akiakizungumza na uongozi wa Garage ya utengenezaji wa Magari ya RSA Limited Mkoani Kilimanjaro
Mkuu wa mkoa wa DEar es salaam Mh. Paul Makonda akikagua moja ya magari 26 ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Dar es salaam yaliyopelekwa katika Garage ya utengenezaji wa Magari ya RSA Limited Mkoani Kilimanjaro.
Hivyo makala MAKONDA ATEMBELEA GEREJI INAYOTENGENEZA MAGARI YA POLISI DAR ES SALAAM YALIYOPELEKWA KUTENGENEZWA.
yaani makala yote MAKONDA ATEMBELEA GEREJI INAYOTENGENEZA MAGARI YA POLISI DAR ES SALAAM YALIYOPELEKWA KUTENGENEZWA. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MAKONDA ATEMBELEA GEREJI INAYOTENGENEZA MAGARI YA POLISI DAR ES SALAAM YALIYOPELEKWA KUTENGENEZWA. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/07/makonda-atembelea-gereji-inayotengeneza.html
0 Response to "MAKONDA ATEMBELEA GEREJI INAYOTENGENEZA MAGARI YA POLISI DAR ES SALAAM YALIYOPELEKWA KUTENGENEZWA."
Post a Comment