MAKAMU WA RAIS AHUDHURIA MKUTANO WA 29 wa UMOJA WA FRIKA MJINI ADDIS ABABA

MAKAMU WA RAIS AHUDHURIA MKUTANO WA 29 wa UMOJA WA FRIKA MJINI ADDIS ABABA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MAKAMU WA RAIS AHUDHURIA MKUTANO WA 29 wa UMOJA WA FRIKA MJINI ADDIS ABABA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MAKAMU WA RAIS AHUDHURIA MKUTANO WA 29 wa UMOJA WA FRIKA MJINI ADDIS ABABA
kiungo : MAKAMU WA RAIS AHUDHURIA MKUTANO WA 29 wa UMOJA WA FRIKA MJINI ADDIS ABABA

soma pia


MAKAMU WA RAIS AHUDHURIA MKUTANO WA 29 wa UMOJA WA FRIKA MJINI ADDIS ABABA

Mkutano wa 29 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU) amefunguliwa rasmi Jijini Addis Ababa- Ethiopia ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli anawakilishwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan katika mkutano huo 

Mkutano huo wa Wakuu wa Nchi na Serikali unaofanyika katika Makao Makuu ya Umoja wa Afrika Jijini Addis Ababa- Ethiopia na utajikita katika kujadili masuala mbalimbali yanayohusu umoja huo ikiwemo hali ya ulinzi na usalama katika Bara la Afrika hasa kwenye nchi za Sudan Kusini, Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo- DRC na Libya.

Aidha, Viongozi hao watajadili hali ya usalama kwenye baadhi ya nchi ambazo ziliathiriwa na kundi la Boko Haram za Nigeria, Niger, Chad na Cameroon.

Wakuu hao wa Nchi na Serikali wa AU pia watajadili kwa kina kuhusu uanzishwaji wa eneo huru la kibiashara katika bara la Afrika kwa ajili ya kuliendeleza Bara hilo kwa ajili ya kukuza biashara baina ya nchi wanachama, uwekezaji, kuondoa vikwazo vya kibiashara pamoja na kupunguza utegemezi kwa masoko ya nje.

Mambo mengine yatakayojadiliwa na Viongozi hao ni bajeti ya Umoja huo, mpango mkuu kuhusu hatua za kivitendo za kuzuia mapigano katika Afrika kufikia mwaka 2020, maboresho katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na maboresho ya kitaasisi katika AU.

Kwa upande wa Tanzania, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan anaongoza ujumbe wa Tanzania katika mkutano huo ambao unahudhuriwa pia na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt Augustine Mahiga na Waziri wa Kazi,Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Maudline Cyrus Castico pamoja na Watendaji wengine wa Serikali. Kauli Mbiu ya Mkutano wa mwaka huu ni Kuimarisha Mgawanyiko wa Idadi ya Watu Kupitia Uwekezaji katika Vijana. (Harnessing Demographic Divident Through Investments in the Youth)
Picha ya pamoja 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amemwakilisha Rais wa John Pombe Magufuli katika mkutano wa AU katika Makao makuu ya Umoja huo Addis Ababa- Ethiopia.Mkutano umefunguliwa hii Leo Jijini Addis Ababa- Ethiopia.
Mkutano wa AU katika Makao makuu ya Umoja huo Addis Ababa- Ethiopia uliofunguliwa leo hii eo Jijini Addis Ababa- Ethiopia ukiendelea


Hivyo makala MAKAMU WA RAIS AHUDHURIA MKUTANO WA 29 wa UMOJA WA FRIKA MJINI ADDIS ABABA

yaani makala yote MAKAMU WA RAIS AHUDHURIA MKUTANO WA 29 wa UMOJA WA FRIKA MJINI ADDIS ABABA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MAKAMU WA RAIS AHUDHURIA MKUTANO WA 29 wa UMOJA WA FRIKA MJINI ADDIS ABABA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/07/makamu-wa-rais-ahudhuria-mkutano-wa-29.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "MAKAMU WA RAIS AHUDHURIA MKUTANO WA 29 wa UMOJA WA FRIKA MJINI ADDIS ABABA"

Post a Comment