title : Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Azungumza na Timu ya Madaktari Kutoka Nchini Misri.
kiungo : Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Azungumza na Timu ya Madaktari Kutoka Nchini Misri.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Azungumza na Timu ya Madaktari Kutoka Nchini Misri.
Na. Othman Khamis OMPR.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema mfumo wa Madaktari wa Misri wa kuweka utaratibu wa kutoa huduma za Afya kwa Wananchi wa Tanzania umeanza kuleta matumaini kwa Wananchi walio wengi Nchini.
Alisema utaratibu huo unazingatia uhusiano wa muda mrefu wa Kibalozi uliopo kati ya Misri na Tanzania na Zanzibar kwa ujumla ambao ulianza tokea kupatikana kwa Uhuru wa Tanganyika Mwaka 1961 na ule wa Mapinduzi ya Zanzibar wa Mwaka 1964.
Balozi Seif Ali Iddi alisema hayo Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar wakati akibadilishana mawazo ya Timu ya Madaktari kutoka Hospitali ya Chuo Kikuu cha El –Shady kiliopo Alexandria Nchini Misri waliopo Zanzibar kutoa huduma za upasuaji kwa wagonjwa mbali mbali.
Alisema alisema wakati umefika kwa Uongozi wa Vyuo Vikuu tofauti vya Nchini Misri kuzingatia uongezaji wa fursa za masomo ya juu kwa Wanafunzi wa Tanzania hasa katika sekta ya Afya na Elimu.
Balozi Seif alieleza kwamba hatua hiyo itasaidia kwenda sambamba na uimarishaji wa Sera za Afya na Elimu zilizolenga kuimarisha elimu ya Msingi kwa Wanafunzi pamoja na huduma ya afya ya Msingi hasa Vijijini.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliueleza Ujumbe huo wa Madaktari Tisa wa Hospitali ya Chuo Kikuu cha El – Shady Alexandria Nchini Misri kwamba Zanzibar imeweka mkakati wa kuwa na huduma za Afya ya Msingi kila baada ya Kilomita Tano.
Mapema Kiongozi wa Timu ya Madaktari hao kutoka Hospitali ya Chuo Kikuu cha El – Shady Alexandria Nchini Misri Profesa Saber Waheeb alisema Timu yake tayari imeshatoa huduma za Afya kwa tariban Mara ya Nnne sasa.
Profesa Waheeb alisema Wataalamu wa Timu hiyo hutoa huduma za upasuaji kwa Watoto walioziba njia ya Mkojo, haja kubwa pamoja na uvimbe wa Tumbo wakitarajia kuwafanyia huduma za Upasuaji wagonjwa wasiopungua 38.
Timu hiyo ya Madaktari Mabingwa wa Hospitali ya Chuo Kikuu cha El –Shady kiliopo Alexandria Nchini Misri wanamalizia kutoka huduma hizo katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja Mjini Zanzibar.
Akiiongoza timu hiyo ya Madaktari Mabingwa wa Hospitali ya Chuo Kikuu cha El –Shady kiliopo Alexandria Naibu Waziri wa Afya Mheshimiwa Harous Said Suleiman alisema ujio wa Madaktari hao umeleta faraja kwa wagonjwa mbali mbali ambao wangelazimika kutumia gharama kubwa kupata huduma hizo nje ya Nchi.
Naibu Waziri Harous aliushukuru Uongozi wa Chuo cha El –Shady Alexandria Nchini Misri kupitia Hospitali yake kwa uamuzi wake wa kutenga Wataalamu wa Afya kutoa huduma Zanzibar katika mpango endelevu unaofanyika kila kipindi.
Hivyo makala Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Azungumza na Timu ya Madaktari Kutoka Nchini Misri.
yaani makala yote Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Azungumza na Timu ya Madaktari Kutoka Nchini Misri. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Azungumza na Timu ya Madaktari Kutoka Nchini Misri. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/07/makamu-wa-pili-wa-rais-wa-zanzibar_25.html
0 Response to "Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Azungumza na Timu ya Madaktari Kutoka Nchini Misri."
Post a Comment