title : HAT TRICK 2 ZAPIGWA PEMBA LIGI KUU ZENJ, SASA HILIKA AFUNIKWA KWENYE UFUNGAJI BORA
kiungo : HAT TRICK 2 ZAPIGWA PEMBA LIGI KUU ZENJ, SASA HILIKA AFUNIKWA KWENYE UFUNGAJI BORA
HAT TRICK 2 ZAPIGWA PEMBA LIGI KUU ZENJ, SASA HILIKA AFUNIKWA KWENYE UFUNGAJI BORA
Na: Abubakar Khatib “Kisandu”, Zanzibar.
Mshambuliaji wa timu ya Jamhuri Mwalimu Mohammed leo amefanikiwa kufunga mabao 3 (Hat trick) katika mchezo wa ligi kuu soka ya Zanzibar hatua ya 8 bora na timu yake Jamhuri iliposhinda mabao 5-3 dhidi ya Mwenge kwenye mchezo uliopigwa jioni ya leo katika uwanja wa Gombani Pemba.
Mabao hayo amefunga katika dakika ya 11, 15, 27 ambapo katika mchezo huo huo mshambuliaji wa timu ya Mwenge Abdull Yussuf nae amelipa hat trick baada ya kufunga mabao yote 3 ya Mwenge katika mchezo huo waliopoteza mabao ambayo alifunga dakika ya 33, 37 na 79.
Washambuliaji hao wote wawili kwasasa ndio vinara wa kuzifumania nyavu katika ligi hiyo ambapo wote wakiwa na jumla ya mabao 7 kila mmoja wakifuatiwa na Ibrahim Hamad Hilika wa Zimamoto mwenye mabao 6 baada ya leo kufunga bao moja timu yake ilipotoka sare ya 1-1 dhidi ya JKU kwenye uwanja wa Amaan.
Jumla ya Hat trick tatu mpaka sasa zimeshafungwa katika ligi hiyo zikiwemo mbili za leo pamoja nay a wiki iliyopita iliyofungwa na Hilika wa Zimamoto.
Hivyo makala HAT TRICK 2 ZAPIGWA PEMBA LIGI KUU ZENJ, SASA HILIKA AFUNIKWA KWENYE UFUNGAJI BORA
yaani makala yote HAT TRICK 2 ZAPIGWA PEMBA LIGI KUU ZENJ, SASA HILIKA AFUNIKWA KWENYE UFUNGAJI BORA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala HAT TRICK 2 ZAPIGWA PEMBA LIGI KUU ZENJ, SASA HILIKA AFUNIKWA KWENYE UFUNGAJI BORA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/07/hat-trick-2-zapigwa-pemba-ligi-kuu-zenj.html
0 Response to "HAT TRICK 2 ZAPIGWA PEMBA LIGI KUU ZENJ, SASA HILIKA AFUNIKWA KWENYE UFUNGAJI BORA"
Post a Comment