EngenderHealth WATOA MSAADA WA VIFA TIBA KWA MKOA WA KIGOMA

EngenderHealth WATOA MSAADA WA VIFA TIBA KWA MKOA WA KIGOMA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa EngenderHealth WATOA MSAADA WA VIFA TIBA KWA MKOA WA KIGOMA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : EngenderHealth WATOA MSAADA WA VIFA TIBA KWA MKOA WA KIGOMA
kiungo : EngenderHealth WATOA MSAADA WA VIFA TIBA KWA MKOA WA KIGOMA

soma pia


EngenderHealth WATOA MSAADA WA VIFA TIBA KWA MKOA WA KIGOMA

Na Editha Karlo -Globu ya jamii-Kigoma

SHIRIKA la Kimataifa lisilo la kiserikali la EngenderHealth limetoa msaada wa vifaa tiba chini ya ufadhili wa Bloomberg kwa Mkoa wa Kigoma ili kuboresha huduma za afya ya uzazi.

Akiongea wakati wakukabidhi vifaa hivyo muwakilishi wa shirika la EngenderHealth kutoka makao makuu Dar es Salaam Dkt.Godson Maro alisema kuwa lengo lao ni kuendelea kuboresha huduma za uzazi,ikiwa ni sambamba na kupunguza vifo vya mama na mtoto.

Dkt Maro alivitaja vifaa walivyotoa msaada kuwa ni pamoja na vitanda vya kujifungulia,mashine za kupima mapigo ya moyo ya mtoto,mzani wa kupima uzito,vitanda vya kupumzikia akina mama baada ya kujifungu,mashine ya kupima mapigo ya moyo ya mtoto akiwa tumboni na drip stand vyote vina thamani ya zaidi ya shilingi milioni 374.

"Vifaa hivi vitapelekwa katika zahanati mbalimbali zilizopo Mkoani hapa zenye upungufu wa vifaa tiba pia tutaendelea kushirikiana na serekali kuboresha huduma za afya ili kufikia malengo makubwa ya kupunguza vifo vya mama na mtoto"alisema

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Dkt Paul Chawote alishukuru kwa msaada huo wa vifaa tiba kwani utawasaidia kutatua changamoto mbalimbali walizokuwa wanakutana nazo katika utoaji wa huduma.

Dkt Chawote alisema kuwa vifaa hivyo watavitunza vizuri ili visaidie wananchi wengi na kudumu kwa muda mrefu.

Alisema Mkoa wa Kigoma unachangamoto ya watumishi katika zahanati nyingi na sababu kubwa ni mbiundombinu hasa ya. barabara hali inayofanya watumishi wengi wakipangiwa kazi huwa hawafiki.

Muwakilishi wa shirika la kimataifa lisilo la kiserekali la EngenderHealth Dkt Godson Maro kutoka makao makuu Dar es Salaam akimkabidhi Mganga mkuu wa Mkoa wa Kigoma Dkt Paul Chawote vifaa tiba vilivyotolewa na shirika hilo ili kuboresha huduma ya uzazi kwa mama na mtoto

Kikosi cha wafanyakazi wa shirika lisilo la kiserekali la kimataifa la EngenderHealth kutoka Dar es salaam na Kigomawakiwa katika picha ya pamoja baada ya makabidhino ya vifaa tiba.


Hivyo makala EngenderHealth WATOA MSAADA WA VIFA TIBA KWA MKOA WA KIGOMA

yaani makala yote EngenderHealth WATOA MSAADA WA VIFA TIBA KWA MKOA WA KIGOMA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala EngenderHealth WATOA MSAADA WA VIFA TIBA KWA MKOA WA KIGOMA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/07/engenderhealth-watoa-msaada-wa-vifa.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "EngenderHealth WATOA MSAADA WA VIFA TIBA KWA MKOA WA KIGOMA"

Post a Comment