DKT. SHEIN AFUNGUA TAWI LA BENKI YA CRDB CHAKE CHAKE, PEMBA, LEO

DKT. SHEIN AFUNGUA TAWI LA BENKI YA CRDB CHAKE CHAKE, PEMBA, LEO - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa DKT. SHEIN AFUNGUA TAWI LA BENKI YA CRDB CHAKE CHAKE, PEMBA, LEO, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : DKT. SHEIN AFUNGUA TAWI LA BENKI YA CRDB CHAKE CHAKE, PEMBA, LEO
kiungo : DKT. SHEIN AFUNGUA TAWI LA BENKI YA CRDB CHAKE CHAKE, PEMBA, LEO

soma pia


DKT. SHEIN AFUNGUA TAWI LA BENKI YA CRDB CHAKE CHAKE, PEMBA, LEO

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, ameeleza kuwa miongoni mwa changamoto zinazowakabili wateja wa Benki nyingi hapa nchini ni msongamano wa wateja pamoja na ucheleweshaji huduma na kuitaka Benki ya CRDB kuwa na mikakati katika kupambana na kadhia hiyo. 
Dk. Shein aliyasema hayo leo huko Chake Chake Pemba, katika sherehe ya ufunguzi wa Tawi jipya la Benki ya CRDB likiwa Tawi la 280 ndani ya mtandao wa benki hiyo kutoka matawi 19 iliyokuwa nayo mara tu baada ya kuanzishwa mnamo mwaka 1996. 
Katika hotuba yake, Dk. Shein alisema kuwa wananchi wanaeleza kwamba, miongoni mwa changamoto zinazosababisha msongamano ni kuwa benki za hapa nchini bado haziendani na kasi ya mabadiliko yanayotokea katika sekta ya fedha. 
Alieleza kuwa katika Siku ya Sherehe za Maadhimisho ya Mei Mosi, mwaka huu yaliyofanyika katika viwanja vya Mahonda, Unguja, Wafanyakazi walipendekeza kuwa Serikali ikae na uongozi wa benki mbali mbali ili ione namna ya kupunguza kero hii kubwa ya msongamano na kuchelewa kutolewa huduma, hasa ifikapo mwisho wa mwezi. 
“Leo nimeona ni busara nikuleteeni mawazo hayo ya wafanyakazi, ambao pia, ni baadhi ya wateja wa benki zenu. Wahenga wanasema ‘Mjumbe hauawi’ ndio maana na mimi nimeufikisha ujumbe kama nilivyoambiwa”, alisema Dk. Shen. 
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohanmed Shein (katikati)  akikata utepe kuzindua Tawi la Benki ya RCDB katika Mji wa Chake chake Pemba leo. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mwanajuma Majid Abdalla,akifuatatiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa CRDB  Bw.Ally Hussein Laay na kulia ni  Mkugenzi Mtendaji wa CRDB Dkt. Charles Kimei
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohanmed Shein (kulia) akipeana mkono wa shukurani  na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa CRDB  Bw.Ally Hussein Laay  mara baada ya  kuzindua Tawi la Benki ya RCDB katika Mji wa Chake chake Pemba leo
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohanmed Shein (katikati)  akitia saini kitabu cha wageni alipotembelea katika Ofisi za Benki ya RCDB baada ya kiuzindua rasmi leo (kulia) Meneja wa Tawi la CRDB Chake chake Pemba Nd,Hamadi Abubakar na (kushoto) Waziri wa Ardhi,Maji,Nishati na Mazingira poia akiwa kaimu Waziri wa Fedha na Mipango Salama Aboud Twalib
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohanmed Shein na Meneja wa Tawi la CRDB Chake chake Pemba Nd,Hamadi Abubakar (katikati) pamoja na Viongozi wengine na Wafanyakazi wa Benki hiyo wakiwa katika picha ya pamoja baada ya uzinduzi wa  Tawi la Benki ya RCDB katika Mji wa Chake chake Pemba uliofanyika leo. Picha na Ikulu. 


Hivyo makala DKT. SHEIN AFUNGUA TAWI LA BENKI YA CRDB CHAKE CHAKE, PEMBA, LEO

yaani makala yote DKT. SHEIN AFUNGUA TAWI LA BENKI YA CRDB CHAKE CHAKE, PEMBA, LEO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala DKT. SHEIN AFUNGUA TAWI LA BENKI YA CRDB CHAKE CHAKE, PEMBA, LEO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/07/dkt-shein-afungua-tawi-la-benki-ya-crdb.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "DKT. SHEIN AFUNGUA TAWI LA BENKI YA CRDB CHAKE CHAKE, PEMBA, LEO"

Post a Comment