title : DC WA NAMTUMBO AWAKAMATA WANUNUZI WA MAZAO WASIOFUATA UTARATIBU. .
kiungo : DC WA NAMTUMBO AWAKAMATA WANUNUZI WA MAZAO WASIOFUATA UTARATIBU. .
DC WA NAMTUMBO AWAKAMATA WANUNUZI WA MAZAO WASIOFUATA UTARATIBU. .
Mkuu wa wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma Luckness Amlima amewakamata wanunuzi wawili wa mazao kutoka manispaa ya Songea kwa kununua mazao katika Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo katika kijiji cha Namahoka bila kibali kutoka Halmashauri hiyo.
Wanunuzi hao waliokamatwa ni Omari Fundi na Salumu pili wote kutoka manispaa ya Songea wakinunua mpunga eneo la kilimo cha umwagiliaji katika kijiji cha Namahoka wilayani humo.
Akiwakamata wanunuzi hao Mkuu wa wilaya huyo aliwataka wafanyabiashara hao kuonesha vibali vya kununua mpunga katika eneo hilo ambapo walishindwa kutoa vibali hivyo na ndipo aliamuru washikwe mpaka walipe ushuru pamoja na faini kwa kutofuata utaratibu .
Aidha katika hatua nyingine mkuu wa wilaya huyo aliwataka wakulima katika eneo hilo kutumia fulsa ya kilimo cha umwagiliaji kujipatia kipato na kubadilisha maisha yao na kuacha kuwanufaisha wafanyabiashara ambao wanawanyonya kila mara.
“Sitakubali Serikali imetumia fedha nyingi kujenga miundombinu ya umwagiliaji kwa ajili ya kuwawezesha wakulima walime zao la mpunga kwa vipindi viwili kwa mwaka lakini wafanyabiashara wanajipenyeza kuwakopesha wananchi fedha kwa riba kubwa na kuwafanya wananchi hao kubaki katika hali zao za umaskini na kuwanufaisha wafanyabiashara alisema mkuu wa wilaya huyo.
Omari Silimu (Mamboya ) mkulima katika eneo hilo alimwambia mkuu wa wilaya huyo kuwa ni kweli kuwa wafanyabiashara hao wanawanyonya wakulima kwa kuwakopesha pesa shilingi elfu ishirini mpaka thelathini wakati wa kupanda kwa ahadi ya kulipa mpunga kiasi cha kilo 120 baada ya mavuno ambapo wakati huu wa mavuno kiasi hicho cha mpunga ni shilingi 120,000.
Mhasibu wa mapato Mji mdogo Lusewa alisema kuwa wafanyabiashara hao walikubali kulipa ushuru pamoja na faini kwa kukiuka utaratibu wa ununuzi wa mazao katika halmashauri hiyo na kuwataka wakulima wanaowakaribisha wafanyabiashara kwenye maeneo ya kilimo kwa njia za kinyemera nao watahesabika na kuunganishwa na wafanyabiashara katika kulipa ushuru na faini.
Mkuu wa wilaya aliyevaa kitenge akiwafokea akinamama wanaokubali kuzurumiwa nguvu zao kwa kupewa shilingi elfu thelathini wakati wa kupanda mpunga na kulipa mpunga kiasi cha kilo 120 kila elfu thelathini ambapo kwa sasa wangeweza kupata shilingi 120,000 badala ya shilingi 30,000( Na mpiga picha Yeremias Ngerangera)
Hivyo makala DC WA NAMTUMBO AWAKAMATA WANUNUZI WA MAZAO WASIOFUATA UTARATIBU. .
yaani makala yote DC WA NAMTUMBO AWAKAMATA WANUNUZI WA MAZAO WASIOFUATA UTARATIBU. . Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala DC WA NAMTUMBO AWAKAMATA WANUNUZI WA MAZAO WASIOFUATA UTARATIBU. . mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/07/dc-wa-namtumbo-awakamata-wanunuzi-wa.html
0 Response to "DC WA NAMTUMBO AWAKAMATA WANUNUZI WA MAZAO WASIOFUATA UTARATIBU. ."
Post a Comment