title : WCF YATOA MUONGOZO WA TATHMINI YA UGONJWA NA AJALI KWA MADAKTARI
kiungo : WCF YATOA MUONGOZO WA TATHMINI YA UGONJWA NA AJALI KWA MADAKTARI
WCF YATOA MUONGOZO WA TATHMINI YA UGONJWA NA AJALI KWA MADAKTARI
MFUKO wa Fidia kwa Wafanyakazi, WCF, umetoa muongozo utakaotumiwa na madaktari na watoa huduma za afya, wakati wa kufanya tathmini ya ugonjwa na ajali kwa mfanyakazi aliyepata madhara mahala pa kazi.
Muongozo huo ni miongoni mwa masuala mbalimbali watakayojifunza madaktari wapatao 70 kutoka hospitali 35 za umma na binafsi za jijini Dar es Salaam.
Akizungumza kwenye ufunguzi wa mafunzo hayo, Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw Masha Mshomba, alisema kuwa madaktari ni wadau muhimu sana katika kufanikisha shughuli za Mfuko huo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Emmanuel Humba akifafanua jambo katika ufunguzi wa semina ya siku tano ya kuwapatia muongozo madaktari utakaowawezesha kuotoa huduma za afya, wakati wa kufanya tathmini ya ugonjwa na ajali kwa mfanyakazi aliyepata madhara mahala pa kazi, semina hiyo imefunguliwa rasmi leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Jengo la GEPF, Jijini Dar es salaam.
“Tunataka hawa madaktari wawe na ujuzi wa kutosha utakaowawezesha kufanikisha azma yetu, na tumeamua kuwa mafunzo ya aina hii yatakuwa endelevu ikiwa ni pamoja na kuwapatia muongozo utakaowasaidia kutekeleza majukumu yao ya kufanya tathmini,” alisema.
Alisema kuwa katika jitihada za kuendeleza mafunzo hayo, Mfuko huo una mpango wa kushirikiana na vyuo vikuu nchini katika kutoa huduma hiyo.
Kuhusu wafanyakazi walioripoti matukio ya ajali kazini kwenye Mfuko huo hadi hivi sasa, alisema jumla ya kesi 670 za wafanyaakzi walioumia na kuhitaji matibabu zimepokelewa.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Masha Mshomba akinzungumza katika ufunguzi wa semina ya siku tano ya kuwapatia muongozo madaktari utakaowawezesha kuotoa huduma za afya, wakati wa kufanya tathmini ya ugonjwa na ajali kwa mfanyakazi aliyepata madhara mahala pa kazi, semina hiyo imefunguliwa rasmi leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Jengo la GEPF, Jijini Dar es salaam.
Alisema kuwa wengi wa wafanyakazi waliopatwa na matatizo hayo kazini wanatoka sekta mbali mbali kama migodi, viwanda na usafirishaji. Aliwaomba wafanyakazi walioumia wakiwa kazini kuwasiliana na Mfuko huo ili kuweza kusaidiwa.
Alibainisha kuwa Mfuko umeingia mkataba na watoa huduma za afya kwenye hospitali na vituo vya afya zaidi ya 6,000 nchi nzima ambapo zitahudumia wafanyakazi hao.
Alisema huduma za matibabu zinatolewa kwa mfanyakazi atakayeumia au kuugua kutokana na kazi. Huduma hizo ni ya gari la kubeba wagonjwa, kumuona daktari,upasuaji, uuguzi, dawa, kurudia matibabu itapobidi na kupatiwa viungo bandia.
Alibainisha kuwa wajibu wa mfanyakazi ni pamoja na kuifahamu sheria ya fidia kwa wafanyakazi, (sura 263 marejeo ya mwaka 2015), kutoa taarifa kwa wakati kwa mwajiri au Mkurugenzi Mkuu pindi atakapopatwa na ajali kazini au kubainika kuwa na magonjwa yanayotokana na kazi.
Aliwaomba wafanyakazi hao kutoa ushirikiano pindi wanapotakiwa kufanyiwa uchunguzi wa matibabu, kuzingatia maelekezo yatolewayo na Mamlaka mbali mbali kuhusu usalama mahali pa kazi, kuzingatia sheria, kanuni, taratibu na miongozo mbali mbali kuhusu masuala ya fidia kwa wafanyakazi , kutunza kumbukumbu binafsi zinazohusu masuala ya kazi.
Akifungua mafunzo hayo, Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya WCF, Emmanuel Humba aliwashauri madktari hao kufanya kazi zao kwa weledi zaidi ili kuongeza tija na ufanisi kwa lengo la kuiwezesha sekta hiyo kuongeza wigo wa upana wa huduma.
Bw. Humba alisema kuwa azma ya mfuko huo kuwa na mtandao mkubwa wa watoa huduma za afya nchi nzima ambao watasaidia Mfuko kutoa fidia stahiki kwa mfanyakazi aliyepata maradhi au majeraha wakati akitekeleza wajibu wake kazini.
Baadhi ya Wakurugenzi wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), wakiwa katika semina hiyo.
“Nyie ni wadau muhimu sana katika kutuwezesha sisi kufanya kazi zetu vizuri ninawaombeni mzingatie yote mtakayofundishwa kwenye mafunzo haya na kuongeza weledi wenu ,” alisema.
BOFYA HAPA KWA HABARI NA PICHA ZAIDI
BOFYA HAPA KWA HABARI NA PICHA ZAIDI
Hivyo makala WCF YATOA MUONGOZO WA TATHMINI YA UGONJWA NA AJALI KWA MADAKTARI
yaani makala yote WCF YATOA MUONGOZO WA TATHMINI YA UGONJWA NA AJALI KWA MADAKTARI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WCF YATOA MUONGOZO WA TATHMINI YA UGONJWA NA AJALI KWA MADAKTARI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/06/wcf-yatoa-muongozo-wa-tathmini-ya.html
0 Response to "WCF YATOA MUONGOZO WA TATHMINI YA UGONJWA NA AJALI KWA MADAKTARI"
Post a Comment