title : watatu waokolewa na mmoja akwama katika mgodi wa Nyakavangala, Iringa
kiungo : watatu waokolewa na mmoja akwama katika mgodi wa Nyakavangala, Iringa
watatu waokolewa na mmoja akwama katika mgodi wa Nyakavangala, Iringa
Na Fredy Mgunda, Iringa
Wachimbaji wa madini watatu wameokolewa kati ya wanne waliokuwa wamefukiwa na mchanga katika mgodi wa Nyakavangala, Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela, amethibitisha.
Akizungumza na blog hii Kasesela alisema kuwa jana mida ya saa 1 jioni Duara la mgodi mmoja ulioko Nyakavangala uliporomoka na kufukia wachimbaji wanne.
"Inasemekana wachimbaji hao walikuwa wameingia kuiba kwani duara hilo ni kati ya maduara ambayo Mkuu Wa wilaya ya Iringa Mhe Richard Kasesela aliifungia ili ijengwe nguzo na ngao" alisema Mhe. Kasesela
DC Kasesela alisema kuwa Watu 4 waliingia mgodini baada ya mafundi Wa ujenzi wa Ngao kupumzika kwa vile ni usiku ndipo wachimbaji hao wakaingia mgodini bila ruhusa.
"Hadi sasa tumefanikiwa kuokoa watatu na mpaka sasa huyo mmoja hajaokolewa bado yupo ndani ya mgodi kutokana na changamoto za uokoaji ila juhudi zinaendelea za kumuokoa huyo mmoja" alisema Kasesela
Kasesela alisema kuwa changamoto ilikuwa ni namna ya kumuokoa kwani sehemu iliyokuwa imejifukia juu mwamba mwingine ulionekana kuwa na dalili za kushuka.ikawapasa kujengea kwanza eneo hilo kazi iliyochukua mda mrefu na ndipo waaze kuokoa.kwahiyo tunasubiri hatua nyingine sasa.
"Naendelea kuwaonya wachimbaji wasiendelee na uchimbaji eneo la chini maarufu kama kwenye "vein" mpaka wajenge ngao ili wasihatarishe maisha yao. Wakiendelea na kiburi tutaamua tufunge mgodi" alisema Kasesela.
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela akizungumza na blog hii juu ya kitu kinachoendelea kwenye mgodi wa Nyakavangala.
Hivyo makala watatu waokolewa na mmoja akwama katika mgodi wa Nyakavangala, Iringa
yaani makala yote watatu waokolewa na mmoja akwama katika mgodi wa Nyakavangala, Iringa Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala watatu waokolewa na mmoja akwama katika mgodi wa Nyakavangala, Iringa mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/06/watatu-waokolewa-na-mmoja-akwama-katika.html
0 Response to "watatu waokolewa na mmoja akwama katika mgodi wa Nyakavangala, Iringa"
Post a Comment