title : WANDISHI WAPEWA ELEMU JUU YA MATONE YA VITAMEN A
kiungo : WANDISHI WAPEWA ELEMU JUU YA MATONE YA VITAMEN A
WANDISHI WAPEWA ELEMU JUU YA MATONE YA VITAMEN A
Na Ramadhani Ali – Maelezo Zanzibar.
Mkuu wa Kitengo cha Lishe kutoka Wizara ya Afya Bi. Asha Hassan amesema Zanzibar bado ipo nyuma katika kiwango cha Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) cha kuwapatia matone ya Vitamn A watoto wenye umri kuanzia miaka miwili hadi miaka mitano.
Bi. Asha alieleza hayo katika mkutano na waandishi wa habari kuhusu zoezi la kuwapatia matone ya Vitamen A watoto wenye umri huo lililoanza tarehe 1 Juni ambalo linategemea kumalizika mwishoni mwa mwezi huu kwa awamu ya kwanza mwaka huu na awamu ya pili itafanyika mwezi Disemba.
Alisema Zanzibar hadi hivi sasa imefikia asilimia 82 katika mpango huo wakati kiwango kilichowekwa na Shirika la Afya Ulimwenguni ni asilimia 95.
Alizitaja Wilaya tatu za Mkoa Mjini Magharibi ndizo zenye asilimia ndogo zaidi chini ya asilimia 70 wakati Wilaya ya Kati inaongoza kwa kuwa na zaidi ya asilimia 95.
Alisema Kitengo kimeanzisha utaratibu wa kuwafuata wazazi wanaoishi mbali na vituo vya afya ili kuwapatia watoto matone ya Vitamin A lakini baadhi ya wazazi wamekuwa hawatoi mashirikiano.
Aliwasisitiza wazazi kufanya juhudi kuhakikisha watoto wao wanapata matone hayo kwa vile ni muhimu katika kuimarisha kinga ya mwili dhidi ya maambukizo ya maradhi ikiwemo kuharisha na kutoona vizuri.
Afisa Kitengo cha Lishe Wilaya ya Mjini Fatma Ali Saidi alisema kumekuwa na dhana potofu kwa wananchi hasa wanaoishi mjini kwamba watoto wao hawahitaji matone ya Vitamin A kwa vile wanakula vizuri lakini dhana hiyo sio sahihi.
Alisema utafiti uliofanywa na Kitengo hicho unaonyesha kwamba watoto wenye hali nzuri ya Vitamin A Zanzibar ni asilimia 12 na asilimia 88 iliyobaki wanaupungufu.
Aliwatoa wasi wasi wazazi kuwa hata wale wachache wenye Vitamin A vya kutosha mwilini wanapopewa matone hayo hayana madhara yoyote na wanaweza kutumia.
Washiriki wa mkutano huo walikishauri Kitengo cha Lishe kuongeza kutoa elimu kwa wazazi kwani baadhi yao bado hawajaelewa umuhimu wa matone ya Vitamin A na wengine wanadhani kuwa matone hayo ni sawa na chanjo jambo ambalo sio sahihi.
Hivyo makala WANDISHI WAPEWA ELEMU JUU YA MATONE YA VITAMEN A
yaani makala yote WANDISHI WAPEWA ELEMU JUU YA MATONE YA VITAMEN A Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WANDISHI WAPEWA ELEMU JUU YA MATONE YA VITAMEN A mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/06/wandishi-wapewa-elemu-juu-ya-matone-ya.html
0 Response to "WANDISHI WAPEWA ELEMU JUU YA MATONE YA VITAMEN A"
Post a Comment