title : WADAU WA PSPF WAWATANGAZIA FURSA WASTAAFU WATARAJIWA
kiungo : WADAU WA PSPF WAWATANGAZIA FURSA WASTAAFU WATARAJIWA
WADAU WA PSPF WAWATANGAZIA FURSA WASTAAFU WATARAJIWA
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said, Mwanza
MFUKO wa Pensheni wa PSPF umewaleta poamoja watumishi wa umma kutoka wilaya zote za mkoa wa Mwanza zaidi ya 450, ambao wanatarajiwa kustaafu hivi karibuni ili kuwapatia semina ya mafunzo itakayowawezwesha kujiandaa kustaafu kwa amani.
Katika semina hiyo iliyoanza leo Juni 2, 2017 kwenye ukumbi wa chuo cha BoT Capri-point jijini Mwanza, wadau wa PSPF ambao ni taasisi za fedha nao wametumia fursa hiyo kutangaza fursa mbalimbali ambazo wastaafu hao wanaweza kuzitumia ili kuendeleza maisha yao ya baadaye.
Wadau hao ni pamoja na Mwalimu Commercial Bank, (MCB), NMB, CRDB, TPB na Mfuko wa UTT-AMIS, pia Shirika la Viwanda Vidogovidogo SIDO.
Bw. Lutenganya, akifafanua zaidi huduma zitolewazo na benki ya MCB
Mkurugenzi wa idara ya mikopo benki ya Posta Tanzania, (TPB), Bw. Henry Bwogi, akizoa mada kwa washiriki ambapo alisema, "TPB ndiyo benki kongwe kuliko zote hapa nchini ikiwa na matawi yaliyosambaa kila kona ya nchi na hivyo kuwa rahisi kwa wateja kufikiwa na huduma zake, lakini pia benki hiyo tayari imeonyesha nia ya dhati ya kuwajali wastaaafu ambapo imekwisha toa mikopo ya mabilioni ya shilingi kwa wanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF.
Bi Doris Mlenge, Afisa Masoko wa Mfuko wa UTT-AMIS, akiwapatia vipeperushi vyenye maelezo ya huduma mbalimbali zitolewazo na Mfuko huo. "Kwa mtu yeyote anayetegemea kupata kipato kwa mkupuo kutokana na pensheni au chanzo kingine cha fedha anatakiwa kuwekeza kwenye Mfuko huo ili aweze kupata kipato cha mara kwa mara na akasema kuwekeza kwenye mifuko ya kujikimu kama UTT-AMIS kunatoa faida kubwa ukilinganisha na uwekezaji wa namna hiyo kwenye masoko ya fedha.
Hivyo makala WADAU WA PSPF WAWATANGAZIA FURSA WASTAAFU WATARAJIWA
yaani makala yote WADAU WA PSPF WAWATANGAZIA FURSA WASTAAFU WATARAJIWA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WADAU WA PSPF WAWATANGAZIA FURSA WASTAAFU WATARAJIWA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/06/wadau-wa-pspf-wawatangazia-fursa.html
0 Response to "WADAU WA PSPF WAWATANGAZIA FURSA WASTAAFU WATARAJIWA"
Post a Comment