title : UWT Zanzibar yawataka wanawake kuchangamkia fursa za Uongozi
kiungo : UWT Zanzibar yawataka wanawake kuchangamkia fursa za Uongozi
UWT Zanzibar yawataka wanawake kuchangamkia fursa za Uongozi
NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.
UMOJA wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi Tanzania (UWT) umewataka wanawake kuchangamkia fursa za Uongozi wa ngazi mbali mbali kupitia uchaguzi unaondelea hivi sasa ndani ya Chama na jumuiya zake.
Wito huo umetolewa Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja huo Zanzibar Bi.Tunu Juma Kondo katika mwendelezo wa ziara ya UWT ya kuzungumza na Viongozi wapya wa ngazi za matawi wa umoja huo uko Jimbo la Kijini Wilaya ya Kaskazini "A" kichama Unguja.
Awambia Akina Mama hao kuwa Uchaguzi wa ngazi mbali mbali unaoendelea katika taasisi hiyo ndio fursa moja wapo ya wanawake kupata nafasi za uongozi ili waweze kufikia malengo ya kupata uwakilishi wa viongozi wenye idadi sawa na wanaume ndani ya Chama hicho.
Alifafanua kuwa wanawake wanatakiwa kuondokana na dhana ya kuendelea kuongozwa kwa kila nafasi za uongozi ndani ya CCM bali wanatakiwa kujiongeza kwa kuwania wenyewe uongozi ndani ya chama hicho ili kuleta maendeleo endelevu ndani ya chama na jumuiya zake.
Pia alisisitiza viongozi hao kuwa pamoja na majukumu ya kiuongozi waliyonayo ni lazima wawahamasishe kwa wingi wanawake kuwania nafasi za uongozi ili kupata viongozi makini na wenye uwezo wa kwenda na kasi za kiutendaji za chama hicho.
"Wanawake wenzangu tutumieni fursa ya Uchaguzi wa Chama kuwania nafasi mbali mbali za uongozi , tusisubiri nafasi za uteuzi bali tusimame wenyewe kupambana kwa kuhakikisha nasi tunakuwa na nyadhifa za uongozi kama walivyo wanaume kwani tunaweza wenyewe bila ya kuwezeshwa’’,. Alisema Bi.Tunu.
Kaimu Naibu Mkuu wa UWT Zanzibar, Bi. Tunu Juma Kondo akizungumza na viongozi wa Matawi ya Jimbo Kijini Wilaya ya Kaskazini “A” kichama Unguja.
Katibu Msaidizi wa Idara ya Organazesheni UWT Zanzibar, Bi. Mgeni Ottow akitoa nasaha kwa viongozi wa Matawi ya Jimbo Kijini Wilaya ya Kaskazini “A” kichama Unguja.
Baadhi ya viongozi wa UWT wa Matawi jimbo la kijini Wilaya ya Kaskazini “A” kichama Unguja wakisikiliza kwa makini nasaha zinazotolewa na viongozi wa UWT Zanzibar uko Tawi la CCM Muange.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala UWT Zanzibar yawataka wanawake kuchangamkia fursa za Uongozi
yaani makala yote UWT Zanzibar yawataka wanawake kuchangamkia fursa za Uongozi Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala UWT Zanzibar yawataka wanawake kuchangamkia fursa za Uongozi mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/06/uwt-zanzibar-yawataka-wanawake.html
0 Response to "UWT Zanzibar yawataka wanawake kuchangamkia fursa za Uongozi"
Post a Comment