Umisseta Zanzibar watua Mwanza

Umisseta Zanzibar watua Mwanza - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Umisseta Zanzibar watua Mwanza, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Umisseta Zanzibar watua Mwanza
kiungo : Umisseta Zanzibar watua Mwanza

soma pia


Umisseta Zanzibar watua Mwanza



Na: Abubakar Khatib Kisandu, Mwanza.

Msafara wa wanamichezo 135 kutoka  Zanzibar  ambao unashiriki mashindano ya umoja wa Michezo na Sanaa skuli za sekondari Tanzania (UMISSETA) umewasili Butimba mjini Mwanza tayari kwa mashindano hayo.
 

Msafara huo uliondoka Zanzibar juzi Jumamosi Juni 3 na kuwasili Mwanza leo asubuhi  wakiwa katika hali nzuri kiafya, na tayari wameanza  kufanya mazoezi madogo kwa ajili ya kuweka miili yao sawa.

Akizungumza na Mtandao huu jijini hapa, Mkuu wa msafara Abdalla Makame Makame ambaye pia ni afisa Elimu Mkoa wa Kusini Unguja, amesema kuwa licha ya safari refu lakini wanamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kufika  salama safari yao hiyo.

‘’Tunashukuru  tumefika salama hapa Mwanza, tumepokelewa vizuri tunachosubiri hivi sasa ni kuanza kwa mashindano, na hapa tumefikia sehemu nzuri  hivyo hatuna  hofu yoyote’’. Alisema Makame.

Akizungumza kwa niaba ya makocha wa michezo kocha awa timu ya mpira wa mikono (handball) Salum Hassan, amesema kuwa vijana wote wapo katika hali nzuri na wapo tayari kwa mashindano.

Amesema kuwa baada ya kufika jioni leo wataanza kufanya mazoezi kwa ajili ya kuweka sawa miili yao, na hali ya hewa ni nzuri haina tofauti sana na hali ya hewa ya nyumbani Zanzibar.

‘’Jioni tutafanya mazoezi leo na kesho tunasubiri ratiba ili tujuwe tumepangwa na nani, lakini kiujumla timu zote zipo vizuri na hali ya hewa ya hapa haina tofauti kubwa sana ila hapa jua ni kali sana’’.Alisema.

Hivyo amezidi kuwaomba Wazanzibari kuendelea kuwaombea dua waweze kucheza  vizuri na hatimae kurudi na makombe mengi .

Katika Mashindano hayo ambayo yanatarajiwa kuanza kutimua vumbi lake kesho Jumanne June 6, 2017 huko Butimba Chuo cha Ualimu Mkoani Mwanza, Zanzibar itakuwa na kanda mbili tofauti Unguja timu yao na Pemba timu yao, ambapo kanda ya Unguja itakuwa na timu za Soka, Wavu, Mikono, Riadha, Mpira wa Meza na Kikapu,wakati kanda ya Pemba itakuwa na timu za Riadha, Wavu, Kikapu na Soka.


Hivyo makala Umisseta Zanzibar watua Mwanza

yaani makala yote Umisseta Zanzibar watua Mwanza Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Umisseta Zanzibar watua Mwanza mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/06/umisseta-zanzibar-watua-mwanza.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Umisseta Zanzibar watua Mwanza"

Post a Comment