TGGA YAENDESHA KAMBI YA MAFUNZO YA MTOTO WA KIKE KUJIAMINI, KUJITAMBUA NA KUWA JASIRI

TGGA YAENDESHA KAMBI YA MAFUNZO YA MTOTO WA KIKE KUJIAMINI, KUJITAMBUA NA KUWA JASIRI - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa TGGA YAENDESHA KAMBI YA MAFUNZO YA MTOTO WA KIKE KUJIAMINI, KUJITAMBUA NA KUWA JASIRI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : TGGA YAENDESHA KAMBI YA MAFUNZO YA MTOTO WA KIKE KUJIAMINI, KUJITAMBUA NA KUWA JASIRI
kiungo : TGGA YAENDESHA KAMBI YA MAFUNZO YA MTOTO WA KIKE KUJIAMINI, KUJITAMBUA NA KUWA JASIRI

soma pia


TGGA YAENDESHA KAMBI YA MAFUNZO YA MTOTO WA KIKE KUJIAMINI, KUJITAMBUA NA KUWA JASIRI



Na Richard Mwaikenda

MAFUNZO ya kujiamini na kujitambua kwa mtoto wa kike yamepamba moto katika kambi maalumu inayoendelea eneo la Mombasa, Ilala, Dar es Salaam.

Kambi hiyo iliyoandaliwa na Chama cha Tanzania Girl Guides (TGGA), inashirikisha walimu na viongozi wa chama hicho kutoka mikoa mbalimbali nchini.

Akizungumza na mwandishi wetu aliyetembelea kambi hiyo leo,Kamishna wa TGGA,Mkoa wa Tanga, Modesta Mshata alisema kuwa lengo la kambi hiyo ni kuwajengea uwezo walimu na viongozi wa kujiamini na kujitambua.

"Tunata mtoto wa kike popote alipo ajiamini, ajitambue na kuwa jasiri ikiwemo pia kumudu maisha kwa kushirikiana vyema na jamii inayomzunguka."Alisema Mshata.

Pia alisema kuwa, lengo ni kumfundisha mtoto wa kike kuwa mama na kiongozi bora wa familia na taifa kwa ujumla. Washiriki 36 wa kambi hiyo ya siku tano wanatoka Kondoa, Dodoma, Tanga, Lindi, Rukwa na Dar es Salaam pamoja na nchi za Uganda, Rwanda na Madagascar.

Washiriki wa Kambi ya Mafunzo ya kuwajengea uwezo wanawake wakiimba  wimbo wa Taifa baada ya kujifunza jinsi ya kufunga kamba vifundo na kupandisha bendera ya Taifa katika kambi ya siku tano iliyoandaliwa na Tanzania Girl Guides Association (TGGA), Mombasa, Dar es Salaam
Wakiimba wimbo wa Taifa

Walimu na viongozi wa chama cha Tanzania Girl Guides (TGGA), wakijenga mahema kwa ajili ya kambi ya kumjengea uwezo mtoto wa kike yaliyoandaliwa na TGGA, Mombasa, Dar es Salaam jana. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG

Wakijifunza kufunga vifundo kwenye mti.



Hivyo makala TGGA YAENDESHA KAMBI YA MAFUNZO YA MTOTO WA KIKE KUJIAMINI, KUJITAMBUA NA KUWA JASIRI

yaani makala yote TGGA YAENDESHA KAMBI YA MAFUNZO YA MTOTO WA KIKE KUJIAMINI, KUJITAMBUA NA KUWA JASIRI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala TGGA YAENDESHA KAMBI YA MAFUNZO YA MTOTO WA KIKE KUJIAMINI, KUJITAMBUA NA KUWA JASIRI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/06/tgga-yaendesha-kambi-ya-mafunzo-ya.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "TGGA YAENDESHA KAMBI YA MAFUNZO YA MTOTO WA KIKE KUJIAMINI, KUJITAMBUA NA KUWA JASIRI"

Post a Comment