TADB YAKUTANA NA WADAU WA KILIMO KUJADILI MIKAKATI YA KUBORESHA UWEZESHAJI KWENYE KILIMO NA VIWANDA

TADB YAKUTANA NA WADAU WA KILIMO KUJADILI MIKAKATI YA KUBORESHA UWEZESHAJI KWENYE KILIMO NA VIWANDA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa TADB YAKUTANA NA WADAU WA KILIMO KUJADILI MIKAKATI YA KUBORESHA UWEZESHAJI KWENYE KILIMO NA VIWANDA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : TADB YAKUTANA NA WADAU WA KILIMO KUJADILI MIKAKATI YA KUBORESHA UWEZESHAJI KWENYE KILIMO NA VIWANDA
kiungo : TADB YAKUTANA NA WADAU WA KILIMO KUJADILI MIKAKATI YA KUBORESHA UWEZESHAJI KWENYE KILIMO NA VIWANDA

soma pia


TADB YAKUTANA NA WADAU WA KILIMO KUJADILI MIKAKATI YA KUBORESHA UWEZESHAJI KWENYE KILIMO NA VIWANDA


Na Mwandishi wetu,
Benki ya Maendeleo ya Kilimo ya Tanzania (TADB) imekutana na wadau wa kilimo ili kujadili mikakati ya kuboresha uwezeshaji kwenye kilimo na viwanda katika kuhakikisha Benki hiyo inasaidia sekta ya Kilimo iweze kusukuma dhamira ya Serikali ya kujenga Uchumi wa Viwanda.

Akizungumza katika kikao hicho Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga amesema kuwa Benki imejipanga kuleta matokeo makubwa kwenye mapinduzi ya kilimo na viwanda hasa vya uchakakataji na usindikaji wa mazao ya kilimo.

Bw. Assenga amesema kuwa mipango hii itasaidia upatikanaji wa mali ghafi kwa viwanda vya ndani hivyo kusukuma ndoto ya Serikali kufikia lengo lake la Kujenga Uchumi wa Viwanda na kuhuisha uwekezaji kwenye Viwanda vidogo vidogo na vya kati vya usindikaji na uchakataji wa mazao ya Kilimo na mifugo.

“Benki imejikita kwenye kusaidia Sekta ya Kilimo iweze kusukuma dhamira ya Serikali ya Uchumi wa Viwanda uweze kutoa matunda yaliyokusudiwa ili kuchagiza na kusaidia Mapinduzi ya Kilimo kutoka kilimo cha kujikimu kwenda cha kibiashara ili kuchangia kwenye ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini,” alisema.

Bw. Assenga amesema katika kuhakikisha azma hiyo inatimia TADB imejipanga kutoa elimu ili kuwajengea uwezowakulima na taasisi mbali mbali za fedha pamoja na vyama vya ushirika kuweza kukopa toka TADB pamoja na kushirikiana na wadau mbali mbali kusaidia uwekezaji mkubwa kwenye Sekta ya Kilimo ili iweze kuinua pato la Taifa na kumkomboa Mwananchi.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji huyo ameongeza kuwa TADB imeanza kujiimarisha  na kuchochea mabenki na taasisisi za fedha kuongeza utoaji wa mikopo na fedha zingine kwenye Sekta ya Kilimo ili kuongoza utoaji mikopo ya uongezaji wa thamani katika shughuli za kilimo.

TADB ni taasisi ya serikali ambayo ilianzishwa kwa ajili ya kutatua ufinyu mkubwa wa upatikanaji wa fedha mikopo kwa ajili ya maendeleo ya kilimo nchini ambao ulikuwa unachangiwa kwa kiasi kikubwa na mikopo mingi kutoka taasisi za fedha kuelekezwa zaidi kwenye upande wa biashara za bidhaa; riba kubwa kwenye mikopo ya kilimo; mikopo ya muda mfupi; masharti magumu ya kukopa bila kuzingatia hali halisi ya sekta ya kilimo  na mazao ambayo inaathiriwa kwa kiasi kikubwa na mabadiliko ya hali ya hewa.




Hivyo makala TADB YAKUTANA NA WADAU WA KILIMO KUJADILI MIKAKATI YA KUBORESHA UWEZESHAJI KWENYE KILIMO NA VIWANDA

yaani makala yote TADB YAKUTANA NA WADAU WA KILIMO KUJADILI MIKAKATI YA KUBORESHA UWEZESHAJI KWENYE KILIMO NA VIWANDA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala TADB YAKUTANA NA WADAU WA KILIMO KUJADILI MIKAKATI YA KUBORESHA UWEZESHAJI KWENYE KILIMO NA VIWANDA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/06/tadb-yakutana-na-wadau-wa-kilimo.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "TADB YAKUTANA NA WADAU WA KILIMO KUJADILI MIKAKATI YA KUBORESHA UWEZESHAJI KWENYE KILIMO NA VIWANDA"

Post a Comment