title : SEKTA YA HABARI NCHINI ITAHESHIMIKA IWAPO WANAHABARI WATAJIWEKEA MALENGO YA KUFANYA KAZI KWA AJENDA
kiungo : SEKTA YA HABARI NCHINI ITAHESHIMIKA IWAPO WANAHABARI WATAJIWEKEA MALENGO YA KUFANYA KAZI KWA AJENDA
SEKTA YA HABARI NCHINI ITAHESHIMIKA IWAPO WANAHABARI WATAJIWEKEA MALENGO YA KUFANYA KAZI KWA AJENDA
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Vyombo vya Habari Tanzania { Tanzania Media Foundation – TMF } Bwana Ernest Sungura amesema hadhi ya Sekta ya Habari Nchini itaheshimika na kuaminika zaidi endapo wanahabari wenyewe watajiwekea malengo ya kufanya kazi kwa agenda katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.
Alisema mfumo wa agenda kwa Wanahabari ndio njia pekee itakayosaidia kuamsha ari sambamba na kuibua changamoto zinazokwaza Jamii na kuzipa nguvu za uwajibikaji Taasisi za Umma na hata zile binafsi katika kuwahudumia kwa umakini Wananchi.
Nd. Ernest Sungura Alisema hayo wakati akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kwenye Jengo la Baraza la Wawakilishi Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar akiuongoza Ujumbe wa Viongozi Wanne wa TMF uliokuwepo Zanzibar kwa ziara maalum ya kukagua Maandalizi na Mikakati ya mradi wa kuwapatia Mafunzo Wanahabari wa Zanzibar.
Alisema kupitia Mfuko wa Vyombo vya Habari zipo agenda zilizowahi kuibuliwa na Wanahabari wa Vyombo tofauti Nchini akizitolea mfano vita dhidi ya Dawa za Kulevya, Udhalilishaji wa Kijinsia na ubalozi wa Usalama barabarani ambazo zimesaidia kuleta faraja kwa Jamii na kuzipunguzia matumizi mabovu yasiyo na msingi Serikali zote mbili.
Alieleza kwamba yapo mambo mengi na mazuri ya kujivunia kutokana na kuanzishwa kwa mfumo huo wa agenda jambo ambalo limeziletea sifa Taasisi za Habari kwa Taifa na Wananchi jambo ambalo lilisaidia kuibua changamoto zinazokwaza Serikali na Jamii kwa ujumla.
Bwana Sungura alimueleza Balozi Seif kwamba katika kuwajengea uwezo uliobobea Waandishi wa Habari katika utekelezaji wa kazi zao.
Alisema kuwa tangu kuanzishwa kwake, TMF tayari imeshatoa ruzuku kwa Wanahabari binafsi zaidi ya 600 na taasisi za kutoka kihabari 120 nchini.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar,Balozi Seif Ali Idd akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Vyombo vya Habari Tanzania { Tanzania Media Foundation – TMF } Bwana Ernest Sungura alipokuwa akizungumza nae jambo ofisini kwake.
Hivyo makala SEKTA YA HABARI NCHINI ITAHESHIMIKA IWAPO WANAHABARI WATAJIWEKEA MALENGO YA KUFANYA KAZI KWA AJENDA
yaani makala yote SEKTA YA HABARI NCHINI ITAHESHIMIKA IWAPO WANAHABARI WATAJIWEKEA MALENGO YA KUFANYA KAZI KWA AJENDA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala SEKTA YA HABARI NCHINI ITAHESHIMIKA IWAPO WANAHABARI WATAJIWEKEA MALENGO YA KUFANYA KAZI KWA AJENDA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/06/sekta-ya-habari-nchini-itaheshimika.html
0 Response to "SEKTA YA HABARI NCHINI ITAHESHIMIKA IWAPO WANAHABARI WATAJIWEKEA MALENGO YA KUFANYA KAZI KWA AJENDA"
Post a Comment