title : Rais wa zamani wa Botswana Ketumile Masire afariki dunia
kiungo : Rais wa zamani wa Botswana Ketumile Masire afariki dunia
Rais wa zamani wa Botswana Ketumile Masire afariki dunia
Botswana imetangaza siku tatu za maombolezi ya kitaifa kufuatia kifo cha rais wa zamani wa nchi hiyo, Sir Ketumile Masire, akiwa na miaka 91.
Sir Ketumile, aliongoza taifa hilo kuanzia 1980 hadi 1998, na amekuwa akisifiwa kwa kuchangia pakubwa katika kuweka msingi imara wa uthabiti wa kisiasa katika taifa hilo, shirika la AFP linasema.Alishiriki pia katika mikakati ya kufanikisha amani katika mataifa kadha Afrika, ikiwa ni pamoja na kufikisha kikomo vita vya wenyewe kwa wenyewe vya muda mrefu nchini Msumbiji.
Sir Ketumile alistaafu 1998 baada ya kuongoza taifa hilo katika kipindi cha ukuaji mkubwa wa kiuchumi na usimamizi mwema wa utajiri wa almasi wa Botswana.Aidha, alishiriki katika kuunga mkono vita dhidi ya serikali ya ubaguzi wa rangi Afrika Kusini na kuunga mkono pia harakati za kupigania uhuru katika mataifa mengine ya kanda hiyo.
Kama kiongozi mstaafu, alishiriki katika juhudi za upatanisho kote Afrika, ikiwa ni pamoja na nchini Kenya, Lesotho, Swaziland na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.Sir Ketumile alikuwa pia mwenyekiti wa Jopo la Kimataifa la Watu Wastahiki ambalo lilichunguza mauaji ya kimbari ya Rwanda ya mwaka 1994. CHANZO BBC
Hivyo makala Rais wa zamani wa Botswana Ketumile Masire afariki dunia
yaani makala yote Rais wa zamani wa Botswana Ketumile Masire afariki dunia Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Rais wa zamani wa Botswana Ketumile Masire afariki dunia mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/06/rais-wa-zamani-wa-botswana-ketumile.html
0 Response to "Rais wa zamani wa Botswana Ketumile Masire afariki dunia"
Post a Comment