Rais Magufuli Atoa Neno Kwa Watumishi wa Uma

Rais Magufuli Atoa Neno Kwa Watumishi wa Uma - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Rais Magufuli Atoa Neno Kwa Watumishi wa Uma, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Rais Magufuli Atoa Neno Kwa Watumishi wa Uma
kiungo : Rais Magufuli Atoa Neno Kwa Watumishi wa Uma

soma pia


Rais Magufuli Atoa Neno Kwa Watumishi wa Uma

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli leo wakati akizindua Mfumo wa serikali wa ukusanyaji kodi kwa njia ya Kieletroniki amewachana baadhi ya watumishi wake akisema wamekuwa wakiwaza mambo makubwa ambayo wanashindwa hata kuyatimiza.

Rais Magufuli amesema kuwa watumishi wengi wamekuwa si wabunifu katika kuangalia vyazo vya mapato ambavyo vinaweza kusaidia serikali kuingiza pesa nyingi lakini wao wamekuwa wakiwaza kuongeza bei ya pombe tu na kuacha vitu vingine ambavyo vingeweza kuongeza mapato kwa serikali kwa njia nyingine nzuri.

"Saizi watu wanahangaika na Machinga wakati tungeweza kutengeneza vitambulisho vya wamachinga na kila kimoja tukauza labda elfu kumi, Machinga akinunua kitambulisho hicho anatambulika na serikali na kinaeleza kuwa anapaswa kuwa wapi, je, ni shilingi ngapi tungezipata hapo kwa idadi wa wamachinga waliopo nchi nzima? Lakini watu wetu wao wanawaza kuongeza bei ya pombe tu, yaani tuna watu wa uchumi wengi lakini sijui hata wanafikiria nini " alisema Rais Magufuli

Mbali na hilo Rais Magufuli alisema hata tabia ya watu kukwepa kulipa kodi inasababishwa na mipango mibovu akitolea mfano kuwekwa bei juu ya kodi ya majengo jambo ambalo linafanya watu wengine kushindwa kulipa kodi hiyo na serikali kupoteza mapato.

"Watu wetu hawa hata kwenye kodi ya majengo unakuta wameweka mtu alipe milioni mbili sasa hizo pesa wananchi wanazipata wapi? Ndiyo maana wanakwepa kodi sababu hawana pesa hizo lakini kama wangeweka labda elfu kumi, ishirini mpaka hamsini halafu wenye maghorofa labda laki mbili ungeona kila mtu angekimbilia yeye mwenyewe kulipa kodi, kwa nyumba zote zilizopo Tanzania tungepata shilingi ngapi? Lakini wameweka pesa kubwa na hawazipati sababu watu hawalipi hawana hizo pesa" alisisitiza Rais Magufuli

Katika hatua ya mwisho Rais Magufuli aliyaomba makampuni ya simu nchini yawe mfano wa kuingwa na ikiwezekana yawe ya kwanza kabisa kujiunga katika mfumo huu mpya wa ukusanyaji wa kodi kwa njia ya kieletroniki kwani mfumo huu una manufaa kwa wawekezaji na Watanzania kwa ujumla.


Hivyo makala Rais Magufuli Atoa Neno Kwa Watumishi wa Uma

yaani makala yote Rais Magufuli Atoa Neno Kwa Watumishi wa Uma Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Rais Magufuli Atoa Neno Kwa Watumishi wa Uma mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/06/rais-magufuli-atoa-neno-kwa-watumishi.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "Rais Magufuli Atoa Neno Kwa Watumishi wa Uma"

Post a Comment