title : POLISI WATOA TAHADHARI MATAPELI WA AJIRA
kiungo : POLISI WATOA TAHADHARI MATAPELI WA AJIRA
POLISI WATOA TAHADHARI MATAPELI WA AJIRA
Mwambawahabari
Katika siku za hivi karibuni, kumeibuka kikundi kidogo cha matapeli wanaozunguka katika maeneo mbalimbali hususani vijijini na kuwalaghai vijana kwamba wao ni watumishi ama waajiriwa wa Jeshi la Polisi na kujipatia fedha kutoka kwa wananchi/vijana hao kwa udanganyifu kwamba watawapatia ajira ndani ya Jeshi la Polisi jambo ambalo siyo la kweli.
Jeshi la Polisi nchini, linatoa tahadhari kwa wananchi kwamba ndani ya Jeshi la Polisi hakuna ajira zilizotangazwa, na hivyo tunawataka wananchi wote kuwa makini na mtandao huo wa matapeli. Mfumo wa ajira ndani ya Jeshi la Polisi ni wa wazi na una utaratibu maalum ambao hutangazwa kwa wananchi kwa mujibu wa taratibu za Jeshi la Polisi.
Kufuatia hali hiyo, Jeshi la Polisi linatoa onyo kali kwa wote wenye tabia hiyo ya utapeli kuacha mara moja na endapo mtu yeyote atabainika hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
Jeshi la Polisi linatoa rai kwa wananchi wote wenye taarifa za matapeli hao kuzifikisha haraka katika kituo chochote cha Polisi kilicho karibu ili sheria iweze kuchukua mkondo wake.
Imetolewa na:
Advera John Bulimba – ACP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.
Makao Makuu ya Polisi.
Hivyo makala POLISI WATOA TAHADHARI MATAPELI WA AJIRA
yaani makala yote POLISI WATOA TAHADHARI MATAPELI WA AJIRA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala POLISI WATOA TAHADHARI MATAPELI WA AJIRA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/06/polisi-watoa-tahadhari-matapeli-wa-ajira.html
0 Response to "POLISI WATOA TAHADHARI MATAPELI WA AJIRA"
Post a Comment