MRADI WA HIPZ WAANDAA MBIO ZA BASKELI KUKUSANYA FEDHA KWA AJILI YA KUIMARISHA HUDUMA ZA AFYA HOSPITALI YA MAKUNDUCHI NA KIVUNGE

MRADI WA HIPZ WAANDAA MBIO ZA BASKELI KUKUSANYA FEDHA KWA AJILI YA KUIMARISHA HUDUMA ZA AFYA HOSPITALI YA MAKUNDUCHI NA KIVUNGE - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MRADI WA HIPZ WAANDAA MBIO ZA BASKELI KUKUSANYA FEDHA KWA AJILI YA KUIMARISHA HUDUMA ZA AFYA HOSPITALI YA MAKUNDUCHI NA KIVUNGE, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MRADI WA HIPZ WAANDAA MBIO ZA BASKELI KUKUSANYA FEDHA KWA AJILI YA KUIMARISHA HUDUMA ZA AFYA HOSPITALI YA MAKUNDUCHI NA KIVUNGE
kiungo : MRADI WA HIPZ WAANDAA MBIO ZA BASKELI KUKUSANYA FEDHA KWA AJILI YA KUIMARISHA HUDUMA ZA AFYA HOSPITALI YA MAKUNDUCHI NA KIVUNGE

soma pia


MRADI WA HIPZ WAANDAA MBIO ZA BASKELI KUKUSANYA FEDHA KWA AJILI YA KUIMARISHA HUDUMA ZA AFYA HOSPITALI YA MAKUNDUCHI NA KIVUNGE



Na Ramadhani Ali – Maelezo Zanzibar

Mradi wa Kuimarisha huduma za Afya Zanzibar (HIPZ) unatarajia kukusanya zaidi ya dola za Marekani 25,000 kwa ajili ya kusaidia huduma za afya katika Hospitali ya Makunduchi na Kivunge ambazo wanazisaidia.
Fedha hizo zitapatikana kufuatia kuandaa resi za baiskeli za kilomita 300 (Bike Ride 2017) katika mikoa mitatu ya Unguja yatakayo dumu kwa muda wa siku sita kuanzia leo.

Akizungumza na waandishi wa habari Hoteli ya Tembo, Mratibu wa resi hizo Dkt. Jon Rees kutoka Uingereza  amesema jumla ya wapanda baiskeli 25 kutoka Ulaya na Zanzibar wanashiriki.

Amesema fedha hizo zitachangwa na makampuni ya ndani na nje ya nchi  na zitatumika kuimarisha huduma za afya hasa  afya ya mama na mtoto katika Hospitali za Kivunge na Makunduchi.

Amesema Resi hizo ambazo ni mara ya tatu kufanya  Zanzibar zilianzia Mji Mkongwe kuzunguka maeneo mbali mbali ya Mkoa Mjini Magharibi zitapitia Nungwi, Makunduchi, Kizimkazi na zitrejea Mji Mkongwe.

Dkt. Ress amewataka wananchi wa Zanzibar kuwaunga mkono na kuwatia hamasa wapanda baiskeli hao hasa katika sehemu watakazopita.Akizindua resi hizo, Mkurugenzi Kinga na Elimu ya Afya Dkt. Fadhil Abdalla Mohd amesema Mradi wa HIPZ  umeleta mafanikio makubwa katika ubunifu wake wa kutafuta fedha kwa ajili ya  huduma za afya kwa kuanzisha mbio hizo.

Amesema pamoja na kukusanya fedha kwa ajili ya huduma za afya pia mbio hizo ni sehemu ya kuwashawishi vijana kufanya mazoezi ambayo ni moja ya njia ya kujikinga na maradhi yasiyoambukiza.

Dkt. Fadhil amesema wakati serikali ipo katika mpango wa kuzipandisha daraja Hospitali ya Makunduchi na Kivunge kuwa za Mkoa, fedha hizo zitatumika kuanzisha majengo mapya na kuimarisha huduma za afya.
MBI1
Mratibu wa resi za baskeli (Bike Ride 2017) Dkt. Jon Rees akizungumza na waandishi wa habari kuhusu dhamira ya mbio hizo Zanzibar ikiwa ni mara yake ya tatu.
MBI2
Mkurugenzi Kinga na Elimu ya Afya Zanzibar Dkt. Fadhil Abdalla Mohd akizungumza na washiriki wa resi za baskeli kabla ya kuanza rasmi  zikiwa na lengo la kuimarisha huduma za afya Hospitali ya Kivunge na Makunduchi.
MBI3
Picha ya pamoja ya washiriki wa Bike Ride 2017 wakifurahia mbio hizo kabla ya kuanza rasmi.
MBI5
Washiriki wa resi za baskeli (Bike Ride 2017) wakikata maeneo ya  viwanja vya Maisra kuendelea na safari yao itakayochukua sita sita.
Picha na Makame Mshenga.


Hivyo makala MRADI WA HIPZ WAANDAA MBIO ZA BASKELI KUKUSANYA FEDHA KWA AJILI YA KUIMARISHA HUDUMA ZA AFYA HOSPITALI YA MAKUNDUCHI NA KIVUNGE

yaani makala yote MRADI WA HIPZ WAANDAA MBIO ZA BASKELI KUKUSANYA FEDHA KWA AJILI YA KUIMARISHA HUDUMA ZA AFYA HOSPITALI YA MAKUNDUCHI NA KIVUNGE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MRADI WA HIPZ WAANDAA MBIO ZA BASKELI KUKUSANYA FEDHA KWA AJILI YA KUIMARISHA HUDUMA ZA AFYA HOSPITALI YA MAKUNDUCHI NA KIVUNGE mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/06/mradi-wa-hipz-waandaa-mbio-za-baskeli.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "MRADI WA HIPZ WAANDAA MBIO ZA BASKELI KUKUSANYA FEDHA KWA AJILI YA KUIMARISHA HUDUMA ZA AFYA HOSPITALI YA MAKUNDUCHI NA KIVUNGE"

Post a Comment