title : Mamadou Sakho atembelea kituo cha SOS Mombasa kwa mchina
kiungo : Mamadou Sakho atembelea kituo cha SOS Mombasa kwa mchina
Mamadou Sakho atembelea kituo cha SOS Mombasa kwa mchina
Mcherzaji wa timu ya Livepool ya Uingereza Mamadou Sakho alipokuwa kituo cha SOS akiwa na mkewe Majda na watoto wake wawili wa kike Aida na Sienna
Mchezaji wa timu ya Livepool ya Uingereza Mamadou Sakho akisalimiana na baadhi ya vijana aliokutana nao katika kituo cha SOS
“BABAANGU ALIKUFA NIKIWA NA MIAKA 12 NA MAISHA YALIKUWA MAGUMU MNO, SASA NINA UWEZO NA MUNGU ATANIULIZA PESA ZANGU NIMEZITUMIA VIPI? LAZIMA NIWASAIDIE WANYONGE
Na: Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.
Leo Saa 8 za mchana katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume ataondoka Beki wa kimataifa wa Ufaransa na kurejea nyumbani, Mamadou Sakho anayechezea Liverpool ya England ambae alikuwepo Visiwani Zanzibar tangu Jumamosi ya June 17, 2017 kwa ziara ya kiutalii ambapo awali ziara hiyo alianzia Tanzania bara kisha kurejea nyumbani Ufaransa na baadae moja kwa moja kufika hapa Zenj.
Lakini mchezaji huyo anaondoka Zanzibar kwa kuwacha ujumbe mzito kwa Wazanzibar baada ya kusema kuwa yeye ni tajiri na anauwezo mkubwa sana lakini binafsi yake anajua fika kuwa akifariki Mwenyezi Mungu atamuuliza utajiri wake ameutumia vipi?
Amesema yeye anauwezo mkubwa wa fedha na muumini wa Dini ya Kiislamu hivyo Mungu atamuuliza fedha zake amezitumia kwa njia gani.
“Mimi fedha ninazo nyingi sana na lakini najua fika kuwa Mungu ataniuliza nimezitumiaje fedha zangu!, nitamjibu vipi nimehonga wanawake!, hapana hivyo lazima nitowe sadaka kwa kuwasaidia watoto Yatima na Masikini na ndio maana nina taasisi yangu maalumu ya kusaidia Mayatima na Masikini”.
Wakati huo huo kumbe Sakho nae alikuwa mtoto yatima na aliishi maisha magumu sana wakati yupo mdogo na anajua umuhimu wa kuwasaidia mayatima ndio maana juzi akaenda kuwasaidia watoto Yatima wa kituo cha SOS Zanzibar.
“Mimi babaangu mzazi alifariki nikiwa na miaka 12, nilikuwa mdogo sana na maisha yangu yalikuwa magumu sana, napenda kuwauliza wanangu AIDA (ana miaka 4) na SIENNA (ana miaka 2) mmezaliwa babaenu anaouwezo mkubwa wa mali kwaiyo na nyinyi mukiwa wakubwa fedha zenu mutafanya nini, basi wananiambia watasaidia masikini na Mayatima, nafurahi sana nikiwasikia hivyo na mimi nazidi kuwasisitiza wawasaidie”.
Sakho alikuwepo Zanzibar pamoja na mke wake anaitwa Majda ambae ana asili ya Moroco pamoja na watoto wao wawili wote wanawake ambao ni AIDA na SIENNA waliozaliwa mwaka 2013 na 2015.
Hivyo makala Mamadou Sakho atembelea kituo cha SOS Mombasa kwa mchina
yaani makala yote Mamadou Sakho atembelea kituo cha SOS Mombasa kwa mchina Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Mamadou Sakho atembelea kituo cha SOS Mombasa kwa mchina mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/06/mamadou-sakho-atembelea-kituo-cha-sos.html
0 Response to "Mamadou Sakho atembelea kituo cha SOS Mombasa kwa mchina"
Post a Comment