KAIMU KATIBU MKUU WIZARA YA MAMBO YA NDANI AWAASA WANACHAMA WA JUMUIYA YA MAENDELEO KUSINI MWA AFRIKA(SADC) KUPAMBANA NA MATENDO YA UHALIFU

KAIMU KATIBU MKUU WIZARA YA MAMBO YA NDANI AWAASA WANACHAMA WA JUMUIYA YA MAENDELEO KUSINI MWA AFRIKA(SADC) KUPAMBANA NA MATENDO YA UHALIFU - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa KAIMU KATIBU MKUU WIZARA YA MAMBO YA NDANI AWAASA WANACHAMA WA JUMUIYA YA MAENDELEO KUSINI MWA AFRIKA(SADC) KUPAMBANA NA MATENDO YA UHALIFU, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : KAIMU KATIBU MKUU WIZARA YA MAMBO YA NDANI AWAASA WANACHAMA WA JUMUIYA YA MAENDELEO KUSINI MWA AFRIKA(SADC) KUPAMBANA NA MATENDO YA UHALIFU
kiungo : KAIMU KATIBU MKUU WIZARA YA MAMBO YA NDANI AWAASA WANACHAMA WA JUMUIYA YA MAENDELEO KUSINI MWA AFRIKA(SADC) KUPAMBANA NA MATENDO YA UHALIFU

soma pia


KAIMU KATIBU MKUU WIZARA YA MAMBO YA NDANI AWAASA WANACHAMA WA JUMUIYA YA MAENDELEO KUSINI MWA AFRIKA(SADC) KUPAMBANA NA MATENDO YA UHALIFU

Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Hassan Simba Yahya, akizungumza wakati wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Kamati Ndogo ya Usalama wa Raia ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), uliofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere, leo jijini Dar es Salaam.

Na Mwandishi Wetu.

Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Hassan Simba Yahya, amewaomba washiriki wa Mkutano wa Kamati Ndogo ya Usalama wa Raia ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), kuhakikisha wanapambana kupunguza vitendo vya ujangili, biashara ya magendo, biashara ya binadamu, uhamiaji haramu kwani vitendo hivyo vinarudisha nyuma maendeleo ya nchi zilizopo katika jumuiya hiyo, hivyo kupelekea kurudi nyuma kwa shughuli za maendeleo na uchumi.

Balozi Simba aliyasema hayo alipozungumza katika Mkutano huo uliojadili masuala mbalimbali ya ulinzi na usalama katika maeneo ya nchi wanachama wa jumuiya hiyo, uliohusu masuala ya uhamiaji, ukimbizi, mbuga na wanyamapori katika maeneo ya nchi wanachama wa jumuiya ya SADC, leo jijini Dar es Salaam.

“Hatuwezi kuendelea kiuchumi katika nchi zetu za wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika, kama matendo ya ujangili,biashara ya binadamu, masuala ya wakimbizi, uhamiaji haramu hayajatafutiwa ufumbuzi, kwani haya yatazorotesha shughuli za kiuchumi ikiwepo utalii, hivyo ni bora tukayafanyia kazi maeneo hayo,” alisema Balozi Simba.

Akizungumza wakati wa uchangiaji mada katika mkutano huo, Mkurugenzi wa Masuala ya Siasa, Ulinzi na Usalama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) Jorge Cardoso, alisema uhalifu katika mipaka ya nchi wanachama ikiwemo uwindaji haramu wa pembe za ndovu, uhamiaji haramu,biashara ya binadamu na madawa ya kulevya lazima vidhibitiwe kwani vikiachwa mbeleni vitahatarisha Amani na utulivu uliopo katika nchi wanachama.

“Amani na utulivu katika nchi wanachama ni kichocheo cha mabadiliko ili kupiga hatua za kimaendeleo kwenda mbele na kushirikiana kukuza uchumi katika nchi wanachama wa SADC, hivyo yatupasa wote kwa pamoja kuunga mkono harakati za kukomesha vitendo vya uhalifu katika nchi na mipaka yetu,” alisema Cardoso.

Aidha washiriki wa mkutano huo kutoka katika nchi za Tanzania, Afrika Kusini, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Swaziland, Malawi, Zimbabwe kwa pamoja walikubaliana kupitia Kamati za Ulinzi na Usalama katika nchi zao kudhibiti matendo yote yanayohatarisha amani na utulivu.
Mkurugenzi wa Masuala ya Siasa,Ulinzi na Usalama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) Jorge Cardoso, akizungumza wakati wa Mkutano wa Kamati Ndogo ya Usalama wa Raia ya Jumuiya hiyo,uliofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere,leo jijini Dar es Salaam.
Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Hassan Simba Yahya, akiongoza Mkutano wa Kamati Ndogo ya Usalama wa Raia ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika,Kulia ni Kamishna Jenerali wa Uhamiaji nchini, Dk. Anna Makakala.Mkutano huo umefanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere,leo jijini Dar es Salaam.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye ,akichangia hoja wakati wa Mkutano wa Kamati Ndogo ya Usalama wa Raia ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika(SADC),uliofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere,leo jijini Dar es Salaam.



Hivyo makala KAIMU KATIBU MKUU WIZARA YA MAMBO YA NDANI AWAASA WANACHAMA WA JUMUIYA YA MAENDELEO KUSINI MWA AFRIKA(SADC) KUPAMBANA NA MATENDO YA UHALIFU

yaani makala yote KAIMU KATIBU MKUU WIZARA YA MAMBO YA NDANI AWAASA WANACHAMA WA JUMUIYA YA MAENDELEO KUSINI MWA AFRIKA(SADC) KUPAMBANA NA MATENDO YA UHALIFU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala KAIMU KATIBU MKUU WIZARA YA MAMBO YA NDANI AWAASA WANACHAMA WA JUMUIYA YA MAENDELEO KUSINI MWA AFRIKA(SADC) KUPAMBANA NA MATENDO YA UHALIFU mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/06/kaimu-katibu-mkuu-wizara-ya-mambo-ya_16.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "KAIMU KATIBU MKUU WIZARA YA MAMBO YA NDANI AWAASA WANACHAMA WA JUMUIYA YA MAENDELEO KUSINI MWA AFRIKA(SADC) KUPAMBANA NA MATENDO YA UHALIFU"

Post a Comment