title : BENKI YA CRDB KUADHIMISHA SIKU YA MTOTO WA AFRIKA KWA WIKI NZIMA NCHINI
kiungo : BENKI YA CRDB KUADHIMISHA SIKU YA MTOTO WA AFRIKA KWA WIKI NZIMA NCHINI
BENKI YA CRDB KUADHIMISHA SIKU YA MTOTO WA AFRIKA KWA WIKI NZIMA NCHINI
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
BENKI ya CRDB imeamua kuadhimisha siku ya Mtoto wa Afrika mwaka huu kwa kutoa elimu kwa wazazi kuhusiana na masuala mbalimbali yanayohusu mtoto ili kuweza kuwajenga vizuri katika malezi.
Siku ya Mtoto Afrika kila mwaka yanadhimishwa Duniani huku Benki ya CRDB ikiadhimisha kwa mwaka wa tano mfululizo ikiwa ni muendelezo wa kuhakikisha watoto na kuwaelimisha wazazi watakaofika katika matawi ya benki huyo..
Akizungumza na waandishi wa habari, MkurugenzI Mtendaji wa CRDB Charles Kimei amesema kuwa wao kama beki ya CRDB wataadhimisha siku ya mtoto wa Afrika katika kila tawi kwani ni siku muhimu kwa kila mtoto nchini kwetu.
"Tutaadhimisha siku ya mtoto Afrika nchini kwetu katika kila tawi la benki yetu pia itakuwa ni siku muhimu sana na kuienzi kwa kuelimisha wazazi masuala mbalimbali ya watoto,"alisema Kimei.
Kimei amesema kuwa,kuanzia kesho itakuwa ni wiki ya ya mtoto wa Afrika katika benki yao na watatoa elimu mbalimbali, kuelimisha wazazi masuala ya watoto pamoja na kuwahamasisha kufungua akaunti ya watoto ya Junior Jumbo.
Mbali na kuwa na elimu mbalimbali zinazohusu watoto, kila tawi la CRDB limejipanga kuhakikisha linatoa huduma nzuri kwa wateja watakaokuja siku ya kesho na wiki nzima kiujumla na hivyo ni katika kuboresha maisha ya mtoto wa kesho.
"Kuwa na wiki hii itakayokuwa inaadhimisha siku ya mtoto wa Afrika na wazazi watapewa elimu kwa watoto wao, pia CRDB wamelenga zaidi katika kusaidia mazingira ya watoto kupitia nyanja ya elimu na kufanya hivyo ni kuboresha maisha ya mtoto wa kesho,"
amesema Kimei.
Amemalizia kwa kusema kuwa wateja watakaojitokeza ndani ya wiki ya mtoto wa Afrika katika matawi ya benki ya CRDB watahudumiwa kipekee na zaidi amewaomba kwenda kwa wingi kupata elimu mbalimbali kuhusu watoto na kuwafungulia akaunti kwa manufaa ya baadae.
MkurugenzI Mtendaji wa CRDB Charles Kimei akizungumza na waandishi wa habari kuelekea siku ya Mtoto wa Afrika itakayoazimishwa siku ya kesho na wao kama CRDB wataiadhimisha kwa wiki nzima ili kutoa elimu kwa wazazi kuhusiana na masuala mbalimbali yanayohusu mtoto ili kuweza kuwajenga vizuri katika malezi.
Waandishi wa habari wakimsikiliza MkurugenzI Mtendaji wa CRDB Charles Kimei.
MkurugenzI Mtendaji wa CRDB Charles Kimei akizungumza na waandishi wa habari kuelekea siku ya Mtoto wa Afrika itakayoazimishwa siku ya kesho na wao kama CRDB wataiadhimisha kwa wiki nzima ili kutoa elimu kwa wazazi kuhusiana na masuala mbalimbali yanayohusu mtoto ili kuweza kuwajenga vizuri katika malezi.
Waandishi wa habari wakimsikiliza MkurugenzI Mtendaji wa CRDB Charles Kimei.
Hivyo makala BENKI YA CRDB KUADHIMISHA SIKU YA MTOTO WA AFRIKA KWA WIKI NZIMA NCHINI
yaani makala yote BENKI YA CRDB KUADHIMISHA SIKU YA MTOTO WA AFRIKA KWA WIKI NZIMA NCHINI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala BENKI YA CRDB KUADHIMISHA SIKU YA MTOTO WA AFRIKA KWA WIKI NZIMA NCHINI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/06/benki-ya-crdb-kuadhimisha-siku-ya-mtoto.html
0 Response to "BENKI YA CRDB KUADHIMISHA SIKU YA MTOTO WA AFRIKA KWA WIKI NZIMA NCHINI"
Post a Comment