WADAU WA MIFUGO WAOMBA ‘SAPOTI’ YA TADB

WADAU WA MIFUGO WAOMBA ‘SAPOTI’ YA TADB - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WADAU WA MIFUGO WAOMBA ‘SAPOTI’ YA TADB, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WADAU WA MIFUGO WAOMBA ‘SAPOTI’ YA TADB
kiungo : WADAU WA MIFUGO WAOMBA ‘SAPOTI’ YA TADB

soma pia


WADAU WA MIFUGO WAOMBA ‘SAPOTI’ YA TADB

Na mwandishi wetu, Arusha

Wadau wa sekta ya mifugo mkoani Arusha wameiomba Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) kuwasaidia katika kuendeleza sekta hiyo kwa kuwapatia mikopo na mahitaji mengine kwa ajili ya kuongeza tija katika ufugaji wa kisasa wa ng’ombe wa nyama na maziwa.

Akizungumza katika kikao cha pamoja kilichofanyika katika Kampuni ya Nyama ya Arusha, kwa niaba ya wafugaji wa mkoa wa Arusha, Kaimu Meneja wa Kiwanda cha Nyama cha Arusha, Bw. Fabian Kissiagi amesema ukosefu na ufinyu mkubwa wa upatikanaji wa fedha za mtaji kwa ajili ya maendeleo ya kilimo hasa katika sekta ya mifugo inawapa changamoto katika uendelezaji wa sekta ya mifugo nchini.

Bw. Kissiagi ameongeza ukosefu wa mikopo ya uhakika inarudisha nyuma ukuaji wa sekta ya mifugo na kurudisha nyuma juhudi za serikali katika kuendeleza sekta ya mifugo.
“Hali ya ukosefu wa mitaji ya uhakika inachangiwa kwa kiasi kikubwa na mikopo mingi kutoka taasisi za fedha kuelekezwa zaidi kwenye upande wa biashara za bidhaa na kutusahau sisi wakulima na wafugaji, hivyo tunaiomba TADB kutusaidia kutatua changamoto hii,” alisema.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga amesema Serikali iliamua kuanzisha Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) ili kusaidia kukabiliana na mapungufu ya wakulima nchini kote ili kuhuisha upatikanaji wa mikopo katika sekta ya kilimo na kuchagiza mapinduzi katika  kilimo nchini.

Bw. Assenga ameongeza kuwa sekta ya mifugo ni mojawapo ya minyororo ya mwanzo inayopatiwa mikopo kwa ajili ya uongezaji wa thamani mazao na mifugo mbalimbali hasa katika uongezaji wa thamani wa ufugaji wa ng’ombe wa nyama na maziwa nchini.

Ameongeza kuwa Benki yake imejipanga kuendeleza uongezaji wa thamani wa Ufugaji wa Ng’ombe wa Nyama na Maziwa.
“Benki inatoa mikopo na kusaidia uwekezaji kwa ajili ya ujenzi, ununuzi wa mitambo na ufungaji wa mitambo ya kuhudumia ng’ombe ikiwemo majosho na mabwawa ya kunyweshea na pamoja na usindikaji wa nyama na maziwa kwa ajili ya kuongeza thamani nyama na maziwa,” alisema Bw. Assenga. 

Naye, Mkurugenzi wa Biashara na Mikopo wa TADB, Bw. Augustino Chacha amesema kuwa TADB inatoa mikopo ya aina tatu ambayo ni Mikopo ya Muda Mfupi (Hadi Miaka Miwili (2)), Mikopo ya Muda wa Kati (Zaidi ya Miaka 2 hadi Miaka Mitano (5)) na Mikopo ya Muda Mrefu (Zaidi ya Miaka 5 hadi Miaka Kumi na Mitano (15)).

“Mikopo hii ni ya riba nafuu ambayo inalenga katika kuchagiza na kusaidia Mapinduzi ya Kilimo kutoka   kilimo cha kujikimu kwenda cha kibiashara ili kuchangia kwenye ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini,” alisema.
Mkoa wa Arusha unashika nafasi ya tatu kati ya mikoa yenye mifugo mingi nchini ambapo inakadiriwa kuwa na zaidi ya ng’ombe, mbuzi na kondoo milioni tatu.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga (aliyesimama) akizungumza katika kikao cha pamoja kati ya TADB na Wadau wa Mifugo mkoani Arusha kuhusu fursa za mikopo ya TADB. Kikao hicho kilifanyika katika Kampuni ya Nyama ya Arusha, jijini Arusha.
Mkurugenzi wa Biashara na Mikopo wa TADB, Bw. Augustino Chacha (aliyesimama) akizungumza kuhusiana na mikopo na huduma zinazotolewa na TADB katika kikao cha pamoja kati ya TADB na Wadau wa Mifugo. Kikao hicho kilifanyika katika Kampuni ya Nyama ya Arusha, jijini Arusha.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI


Hivyo makala WADAU WA MIFUGO WAOMBA ‘SAPOTI’ YA TADB

yaani makala yote WADAU WA MIFUGO WAOMBA ‘SAPOTI’ YA TADB Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WADAU WA MIFUGO WAOMBA ‘SAPOTI’ YA TADB mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/05/wadau-wa-mifugo-waomba-sapoti-ya-tadb.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "WADAU WA MIFUGO WAOMBA ‘SAPOTI’ YA TADB"

Post a Comment