title : VIJANA WAMETAKIWA KUWA WABUNIFU
kiungo : VIJANA WAMETAKIWA KUWA WABUNIFU
VIJANA WAMETAKIWA KUWA WABUNIFU
Mwambawahabari
Mkurugenzi wa Sahara Sparks Jumanne Mtambalike amewataka vijana wa kitanzania kuwa makini na biashara zao mbalimbali wanazozifanya kwa kuziweka kwenye mpangilio ulio bora,kwa lengo la kuwahamasisha wawekezaji kuwekeza kwenye biashara zao.
Akizungumza na waandishi wa habari kwenye mkutano mkubwa wa teknolojia,ubunifu na ujasiriamali hapa nchini,Mtambalike amesema kuwa wameandaa mkutano huo kwa lengo la kukuza fursa za kiteknolojia hapa nchini hasa kwa vijana.
“Nawahasa vijana wakati ni huu kama kulikuwa nawakati mwingine haupo kinachotakiwa nikujipanga vizuri kwenye biashara unayoifanya ili kuwahamasisha wawekezaji kuwekeza ”amesema
Aidha amesema kupitia mkutano huo utasaidia vijana wa kitanzania kuondokana na utegemezi na kuanzisha viwanda vyao vidogovidogo na kutimiza sera na dhana ya serikali katika kufikia Tanzania ya viwanda .
Pia amesema mkutano huo utacwakutanisha washiriki kutoka sehemu mbalimbali za nchi ya Tanzania , Africa na Dunian kwa ujumla kushiriki kwa pamoja na makampuni madogo ya kiteknolojia hapa nchini ikiwa ni pamoja na kuwapatia fursa ya kuonyesha kazi zao wanazozifanya.
“Mkutano huu umeunganisha zaidi ya vijana 1200 ambapo kati yao vijana wapatao 200 wameweza kumiliki kampuni zao wenyewe,nia yetu ni kuwakutanisha na wawekezaji mbalimbali wa ndani na nje ya nchi ili kuangalia ni jinsi gani wataweza kuzikuza biashara zao,pia mkutano huu utaambatana na maonesho makubwa ya teknolojia.
Hivyo makala VIJANA WAMETAKIWA KUWA WABUNIFU
yaani makala yote VIJANA WAMETAKIWA KUWA WABUNIFU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala VIJANA WAMETAKIWA KUWA WABUNIFU mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/05/vijana-wametakiwa-kuwa-wabunifu.html
0 Response to "VIJANA WAMETAKIWA KUWA WABUNIFU"
Post a Comment