Serikali Yakusudia Kujenga Magereza Maeneo ya Kilimo

Serikali Yakusudia Kujenga Magereza Maeneo ya Kilimo - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Serikali Yakusudia Kujenga Magereza Maeneo ya Kilimo, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Serikali Yakusudia Kujenga Magereza Maeneo ya Kilimo
kiungo : Serikali Yakusudia Kujenga Magereza Maeneo ya Kilimo

soma pia


Serikali Yakusudia Kujenga Magereza Maeneo ya Kilimo

Na Nuru Juma-MAELEZO

Serikali inamkakati wa kuhakikisha inajenga Magereza katika maeneo yenye uzalishaji mkubwa wa kilimo ambayo pia yana ukubwa wa kutosha ili kazi ya kuwarekebisha wafungwa iwe rahisi kufanyika huku shughuli za uzalishaji zikiwa zinaendelea.

Hayo yamesemwa leo Bungeni Mjini Dodoma na Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Mhe. Mwigulu Nchemba alipokuwa akijibu swali la Mhe Devotha Minja Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Morogoro. 

“Magereza hayo yatajengwa katika maeneo yenye Kilimo na yatakuwa ni kwa ajili ya watu waliokwisha hukumiwa huku yale Magereza ya mijini yawe kwa ajili ya mahabusu tu ili wawe karibu na Mahakama,”alisema Mwigulu. 

Aliongeza kuwa mkakati huo wa Serikali ni wa muda mrefu na wanahitaji kufanya hivyo ili kurahisisha shughuli za maendeleo zinazofanywa na wafungwa na pia kupunguza msongamano wa wafungwa katika Magereza.

Hili pia linatokana na tamko la Mh.Rais Dkt John Pombe Magufuli alilowahi kulitoa hivi karibuni kuwa wafungwa wako katika kutumikia adhabu hivyo wanatakiwa kufanya kazi hasa za kilimo ili kwanza kujipatia chakula na sio kukaa tu bure na kusubiri kila kitu wafanyiwe na serikali.



Hivyo makala Serikali Yakusudia Kujenga Magereza Maeneo ya Kilimo

yaani makala yote Serikali Yakusudia Kujenga Magereza Maeneo ya Kilimo Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Serikali Yakusudia Kujenga Magereza Maeneo ya Kilimo mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/05/serikali-yakusudia-kujenga-magereza_17.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Serikali Yakusudia Kujenga Magereza Maeneo ya Kilimo"

Post a Comment