SERIKALI KUJENGA DARAJA LA JUU ENEO LA KAWE- BONDENI JESHINI

SERIKALI KUJENGA DARAJA LA JUU ENEO LA KAWE- BONDENI JESHINI - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa SERIKALI KUJENGA DARAJA LA JUU ENEO LA KAWE- BONDENI JESHINI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : SERIKALI KUJENGA DARAJA LA JUU ENEO LA KAWE- BONDENI JESHINI
kiungo : SERIKALI KUJENGA DARAJA LA JUU ENEO LA KAWE- BONDENI JESHINI

soma pia


SERIKALI KUJENGA DARAJA LA JUU ENEO LA KAWE- BONDENI JESHINI


Na Daudi Manongi-MAELEZO, DODOMA. 

Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano imesema itajenga daraja la juu kwa ajili ya kivuko cha waenda kwa miguu(Over head Pedestrian Bridge) eneo la Kawe Bondeni. 

Hayo yamesemwa Bungeni leo na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe.Isack Kamwelwe aliyekuwa akijibu swali la Mbunge wa Kawe Mhe.Halima Mdee kwa Niaba ya Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano. 

“Tatizo la kivuko cha waenda kwa miguu eneo la Kawe Bondeni hadi Jeshini Kata ya Mbezi Juu na Kawe Tayari limeshapatiwa ufumbuzi”,Aliongeza Mhe.Kamwelwe. 

Amesema kwa sasa Mkandarasi wa kujenga daraja hilo yupo kwenye hatua za maandalizi ya kuanza ujenzi katika eneo hilo muhimu. 

Aidha Serikali ina mpango wa kuweka taa za kuongozea magari katika Barabara ya Mwenge-Tegeta ambapo Mkandarasi ameshapatikana wa kuweka taa hizo katika makutano ya Afrikana na anatarajia kuanza kazi wakati wowote. 

Mbali na Hayo tatizo la Udogo wa mapokeo na matoleo ya maji ya mvua yanayosababisha kero katika eneo la Makonde hadi Mbuyuni,Serikali inakamilisha taratibu za kusaini mkataba wa ujenzi wa mtaro mkubwa eneo la Mbezi Samaki ambao utatatua kero ya barabara kujaa maji nyakati za mvua. 

“Serikali ya Awamu ya Tano ni makini sana na itahakikisha changamoto hizi inazifanyia kazi ili wananchi waweze kutumia barabara zetu vyema”Aliongeza Mhe.Kamwelwe.
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe.Isack Kamwelwe


Hivyo makala SERIKALI KUJENGA DARAJA LA JUU ENEO LA KAWE- BONDENI JESHINI

yaani makala yote SERIKALI KUJENGA DARAJA LA JUU ENEO LA KAWE- BONDENI JESHINI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala SERIKALI KUJENGA DARAJA LA JUU ENEO LA KAWE- BONDENI JESHINI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/05/serikali-kujenga-daraja-la-juu-eneo-la.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "SERIKALI KUJENGA DARAJA LA JUU ENEO LA KAWE- BONDENI JESHINI"

Post a Comment