title : RC TABORA APIGA MARUFUKU USAFISHAJI WA TUMBAKU NJE YA WILAYA
kiungo : RC TABORA APIGA MARUFUKU USAFISHAJI WA TUMBAKU NJE YA WILAYA
RC TABORA APIGA MARUFUKU USAFISHAJI WA TUMBAKU NJE YA WILAYA
NI BAADA YA WAKULIMA 18 KUKAIDI AGIZO LA WAZIRI MKUU.· ATAKAYEKAMATWA TUMBAKU YAKE KUTAIFISHWA
Na Tiganya Vincent
RS-Tabora
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Bw. Aggrey Mwanri amepiga marufuku usafirishaji wa tumbaku kutoka Wilaya moja kwenda nyingine ili kudhibiti utoroshaji unaotarajiwa kufanya na baadhi ya wakulima wasio waaminifu ambao hadi hivi sasa wamekaidi agizo la Waziri Mkuu la kuwataka wakulima wote kuuza tumbaku yao kupitia Vyama vya Msingi vilivyopo katika maeneo yao.
Marufuku hiyo inafuatia wakulima wa kujitegemea (IF) zaidi ya 16 kutoka Wilaya ya Urambo na Uyui kukataa kujisajili katika Vyama vya Msingi na hivyo kutoonyesha kuwa watauzia tumbaku yao kupitia Chama gani cha Msingi.
Mkuu wa Mkoa huyo alitoa agizo hilo jana mjini Tabora wakati wa kikao cha wadau wa tumbaku, Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa , ambapo pamoja na mambo mengine kupitia Bodi ya Tumbaku Tanzania kimejadili tarehe ya kuanza kwa masoko ya tumbaku ambayo yataanza siku ya Ijumaa wiki hii (26.5.2017) katika meneo mbalimbali.
Alisema kuwa Serikali iliamua wakulima wote kuuzia tumbaku yao kupitia Vyama vya Msingi katika maeneo yao na sio vinginevyo ili kuepuka watu wanatumia mwanya wa kujitegemea kuwarubuni tumbaku ya wakulima wadogo wadogo walipo katika vyama vya msingi na kuwauzia baadhi ya tumbaku yao na kusababisha madeni katika vyama vyao vya Msingi.
Mkuu huyo wa Mkoa alisema kuwa hadi hivi sasa baadhi ya wakulima hao wamekata kujisajili katika Vyama vya Msingi vilivyopo katika maeneo yao na hata kwingine ni ishara tosha kuwa wanampango wa kutorosha tumbaku hiyo kwenda kuuzia wanakujua kinyume na agizo la Waziri Mkuu.
Alisisitiza kuwa yeye akiwa Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Mkoa , hawezi kukubali watu wakaidi agizo la Waziri Mkuu kwa nia ya kutaka kuwanyonya wakulima wengine.
Kufuatia hali hiyo aliagiza Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa , Wilaya kushirikiana na Watendaji ngazi za chini na kuwakamata wao na mizigo yote itakayokuwa inasafirisha nje ya eneo la Chama cha Msingi la Mkulima anapokaa kama bidhaa hiyo haijanunuliwa na kupata hati inayotambulika na Bodi ya Tumbaku ya Tanzania (TTB) na wanunuzi rasmi wa tumbaku wenye vibali vya kufanya kazi hiyo mkoani Tabora.
Hivyo makala RC TABORA APIGA MARUFUKU USAFISHAJI WA TUMBAKU NJE YA WILAYA
yaani makala yote RC TABORA APIGA MARUFUKU USAFISHAJI WA TUMBAKU NJE YA WILAYA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala RC TABORA APIGA MARUFUKU USAFISHAJI WA TUMBAKU NJE YA WILAYA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/05/rc-tabora-apiga-marufuku-usafishaji-wa.html
0 Response to "RC TABORA APIGA MARUFUKU USAFISHAJI WA TUMBAKU NJE YA WILAYA"
Post a Comment