RAIS MSTAAFU MWINYI AONGOZA MAZISHI YA KITWANA KONDO

RAIS MSTAAFU MWINYI AONGOZA MAZISHI YA KITWANA KONDO - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa RAIS MSTAAFU MWINYI AONGOZA MAZISHI YA KITWANA KONDO, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : RAIS MSTAAFU MWINYI AONGOZA MAZISHI YA KITWANA KONDO
kiungo : RAIS MSTAAFU MWINYI AONGOZA MAZISHI YA KITWANA KONDO

soma pia


RAIS MSTAAFU MWINYI AONGOZA MAZISHI YA KITWANA KONDO

Na. Eliphace Marwa - Maelezo.

RAIS Mstaafu Ali Hassan Mwinyi ameongoza mamia ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam katika maziko ya mwanasiasa mkongwe na aliyekuwa Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Kitwana Kondo.

Mbali na Mwinyi wengine waliohudhuria maziko hayo yaliyofanyika katika makaburi ya Tambaza ni Makamu wa Rais Mstaafu, Mohammed Gharib Bilal, Mawaziri Wakuu Wastaafu, Salim Ahmed Salim na Edward Lowassa, Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana, Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba pamoja na wengine.

Akizungumza nyumbani kwa marehemu, Mzee Mwinyi alisema, marehemu Kondo alikuwa  ni mtu ambaye alijitoa katika kulitumikia taifa kwa moyo wake, hivyo mchango wake ni mkubwa katika kulitumikia taifa na hasa wakazi wa jiji la Dar Es Salaam.

"Alikuwa ni rafiki yangu ambaye tumefahamiana kwa muda mrefu sana, tumepoteza mtu muhimu sana, lakini kazi ya Mungu haina makosa, tumuombee kwa Mwenyezi Mungu amlaze mahali pema peponi," alisema Mzee Mwinyi

Kwa upande wake, Kinana alisema, taifa na hasa wakazi wa Dar es Salaan wamepata pigo kubwa kwa kumpoteza mzee huyo ambaye bado busara zake zilikuwa zikihitajika.

"Alikuwa ni kiongozi wa jamii,alikuwa ni mwalimu wa watu wengi katika manbi mbalimbali, ni msiba mkubwa lakini nj kazi ya Mungu, tuendelee kumuombea apumzike kwa amani," alisema Kinana.

Naye, Waziri Mkuu wa Zamani, Edward Lowassa alisema, kutokana na kazi kubwa iliyofanywa na Mzee Kondo ni vema uongoziu wa jiji kuangalia namna ambavyo barabara moja ya jiji hilo likapewa jina la KK ikiwa ni kuheshimu na kutambua mchango wake.

"Namuomba Mstahiki Meya, barabara moja uiite KK, itakuwa ni heshima kumuenzi Mzee Kitwana Kondo kwa kazi kubwa aliyofanya wakati wa uhai wake," alisema Lowassa.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) , Profesa Ibrahim Lipumba alisema, mchango wa Mzee katika taifa ni mkubwa lakini kwa bahati mbaya ni kama jmeshindwa kutambuliwa.

"Ni mtu ambaye bahati mbaya sana historia ya nchi yetu haitambui mchango wake katika kuleta uhuru wa nchii na kudumisha uhuru wa nchii," alisema Profesa Lipumba.

Akieleza chanzo cha kifo cha baba yake, mtoto wa kwanza wa marehemu Mzee Kondo, Stara Kondo alisema, Baba yake alilazwa katika hospitali ya Hindu Mandal Mei 18 kutokana na kuugua muda mrefu lakini alifariki juzi.

“Alikuwa anaumwa muda mrefu lakini hadi anafariki madaktari walisema alipata stroke (Kiharusi) na shinikizo la damu, tutamkumbuka kwa mambo mengi kwa sababu ni baba lakini alikuwa ni kichwa cha familia,” alisema Stara 
 Mwili wa aliyekuwa Meya wa Jiji la Dar es Salaam na Mbunge wa Kigamboni Kitwana Kondo ukiwa ukiwa umeingizwa kwenye kaburi tayari kwa ajili ya maziko katika makaburi ya Tambaza yaliyopo Upanga jijini Dar es Salaam.
 Rais Mstaafu wa awamu ya pili Dkt. Ali Hassan Mwinyi akiweka udongo katika kaburi la aliyekuwa Meya wa Jiji la Dar es Salaam na Mbunge wa Kigamboni Kitwana Kondo katika makaburi ya Tambaza yaliyopo Upanga jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais Mstaafu Dkt. Mohamed Ghalib Bilal akiweka udongo katika kaburi la aliyekuwa Meya wa Jiji la Dar es Salaam na Mbunge wa Kigamboni Kitwana Kondo katika makaburi ya Tambaza yaliyopo Upanga jijini Dar es Salaam.
 Mwanasiasa mkongwe nchini Kingunge Ngombare Mwilu akiweka udongo katika kaburi la aliyekuwa Meya wa Jiji la Dar es Salaam na Mbunge wa Kigamboni Kitwana Kondo katika makaburi ya Tambaza yaliyopo Upanga jijini Dar es Salaam.
Jaji Mstaafu Mark Bomani akiweka udongo katika kaburi la aliyekuwa Meya wa Jiji la Dar es Salaam na Mbunge wa Kigamboni Kitwana Kondo katika makaburi ya Tambaza yaliyopo Upanga jijini Dar es Salaam.


Baadhi ya wananchi walioshiriki mazishi ya aliyekuwa Meya wa Jiji la Dar es Salaam na Mbunge wa Kigamboni Mzee Kitwana Kondo wakiweka udongo wakati wa mazishi mapema leo jioni jijini Dar es Salaam.

Picha Emmauel Massaka,Globu ya jamii


Hivyo makala RAIS MSTAAFU MWINYI AONGOZA MAZISHI YA KITWANA KONDO

yaani makala yote RAIS MSTAAFU MWINYI AONGOZA MAZISHI YA KITWANA KONDO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala RAIS MSTAAFU MWINYI AONGOZA MAZISHI YA KITWANA KONDO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/05/rais-mstaafu-mwinyi-aongoza-mazishi-ya.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "RAIS MSTAAFU MWINYI AONGOZA MAZISHI YA KITWANA KONDO"

Post a Comment